Watafiti wabaini wapendao sana kujipiga selfie wana tatizo hili kubwa!
Watafiti Wanadai inaweza kuwa ni ishara ya kuwa na matatizo kwenye mahusiano yao au tatizo la afya ya akili.
Wanaojipiga sana selfie wanaweza kuwa watu wenye kasoro au wanaotafuta
kuangaliwa, utafiti umesema. Watafiti nchini Thailand, walifanyia
tathmini wanafunzi 300 na kuangalia mara ngapi huangalia picha
walizojipiga wenyewe.
Washiriki hao ambao wengi walikuwa wanawake, walikuwa na umri kuanzia
miaka 21 hadi 24, walihojiwa kuangaliwa kama walikuwa ni watu wa
kujiamini, kutaka kuonekana, tabia ya kuwa wenyewe au upweke.
Wengi wao walionekana kutumia asilimia 50 ya muda wao wa ziada katika simu zao au kwenye internet.
Wataalam wanaamini kuwa wanaume na wanawake wenye upweke hupenda kuchukua zaidi selfie kutafuta kukubalika na watu wengine.
mgblog
No comments:
Post a Comment