Tangakumekuchablog
Tanga, MWENYEKITI wa mtaa wa Centrol
Tanga, Diana Mussa, amewataka wakazi wa eneo hilo kuweka mazingira ya usafi kwa
kila nyumba ili kuondosha kitisho cha magonjwa ya miripuko na kusema kuwa
ambaye atakaidi agizo hilo atachukuliwa hatua za kisheria.
Akizungumza mara baada ya ufunguzi wa duka la kuuza umeme
la Zola lililopo barabara ya Markert Street Tanga juzi , Diana amesema agizo hilo
litakuwa endelevu na ofisi yake ikiongozwa na yeye kila siku asubuhi atafanya
ukaguzi kwa kila mtaa.
Amesema halmashauri ya jiji imeweka vyombo maalumu vya
kuhifadhia takataka na magari ya kusomba taka mtaani hivyo kutaka kila mmoja
kuhakikisha eneo lake linakuwa katika mazingira mazuri.
Akizungumza kwenye ufunguzi huo,Meneja mauzo kanda ya
Kaskazini Tanga na Kilimanjaro, Peter Laizer, amewataka wajasiriamali
wadogowadogo kutumia umeme wa Zola na kusema kuwa ni wa gharama nafuu.
Amesema Wajasiriamali wa mbogamboga na matunda wanaweza
kuinua kipato chao kwa kusindika na kuweza kusafirisha kwenda katika masoko ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki ambako watajitangaza
tofauti na kutegemea mteja mmoja mmoja.
Amesema umeme huo ni mkombozi kwa watu wa kipato chote, cha
chini, kati na juu na, umeme huo utaondolea adha mbalimbali kama za kuchaji
simu mbali na nyumbani na ufuatiliaji wa taarifa katika Luninga pamoja na kusaidia watoto kusoma katika mwanga
bora nyakati za usiku.
“Umeme huu ni mkombozi
kwa wananchi wa Tanga kwani ni rahisi, hauchukui muda kuupata na pia
utawasaidia wananchi kuhifadhi kiasi cha pesa ambacho walikuwa wanakitumia kwa
nishati nyingine kupata mwanga, Pia humsaidia mwananchi wa kipato cha chini
kubadilisha maisha kwa kupata habari, taarifa pamoja na burudani, kwani mbali
na taa na kuchaji simu pia utapata Radio na TV za sola”alisema Laizer
Alisema umeme huo umekuwa mkombozi kwa wanafunzi wa
vijijini ambao walikuwa hawana uwezo wa kujisomea usiku au husoma katika mwanga
hafifu wa vibatari sasa wanapata mwanga salama kwa afya ya mwili na
macho.
Mwisho
Mwenyekiti wa mtaa wa Centrol Tanga, Diana Mussa, katikati akikata uzi kuashiria ufunguzi wa dula la kuuza umeme wa Zola Markert Street mjini Tanga juzi , kushoto ni Msimamizi wa maduka ya Zola , Bethany Katen na kulia ni Mtendaji kata ya Centrol Bhati Marungu.
Meneja Mauzo kanda ya Kaskazini maduka ya kuuza umeme wa Zola , Pitter Laizer akitoa maelezo ya matumizi wa umeme wa Zola wakati wa ufunguzi wa duka hilo juzi.
Wakazi wa Tanga wakiangalia radio za kuchaji baada ya kuchajiwa kwa kutumia umeme wa Zola wakati wa ufunguzi wa duka la kuuzia umeme wa Mypower Tanga juzi
No comments:
Post a Comment