Thursday, December 29, 2016

AFICHUA SIRI YA KUTAKA KUJIUA

Bondia Ricky Hatton: Nilijaribu kujiua mara kadhaa

Bondia Ricky hatton Kushoto anasema kuwa alijaribu kujiua mara kadhaa kutokana na tatizo la shinikizo la kiakili
Bingwa wa zamani wa dunia na bondia wa Uingereza, Ricky Hatton(Kushoto)  amefichua kuwa alifikiria kujiua mara kadhaa kutokana na shinikizo la akili.
Mwanandondi huyo aliyestaafu mwaka wa 2012, ambaye kwa sasa ni mkufunzi wa mabondia, alieleza kuwa amepitia uchungu mwingi.
"Nilijaribu kujiua mara kadhaa," alisema. "Nilikuwa nikienda kwenye baa, kurudi, nikilia kwenye giza nikiwa nimetoa kisu." "Mwishowe nilihisi kuwa huenda nikajiuwa kwa kulewa kwa sababu nilikuwa na uchungu mwingi".
Hatton ameiambia BBC kuwa kuna umuhimu wa mabondia kupewa ushauri na kusaidiwa wanapostaafu ili kupata nafuu kutoka kwa shinikizo za akili.
"Wanasoka wana maajenti na wasimamizi wanaowasaidia katika vilabu vyao, lakini mabondia, mara tu muda wao unapoisha, unabaki peke yako," alimaliza.
"Kuna mengi yanayofaa kufanywa kuwasaidia mabondia, wengi wetu tanaathirika kwasababu huu mchezo mtu yuko pekee yake na unapostaafu, unaishi maisha ya upweke".
Hatton alipokonywa kibali cha ndondi mwaka wa 2010 baada ya kukiri kutumia mihadarati aina ya 'Cocaine'.
Aidha, ameshinda mapigano 21 yakiwemo kumcharaza bingwa wa dunia wa light-welterweight Kostya Tszyu mjini Manchester mwaka wa 2005 na kuondoka na taji la IBF.
Mwaka wa 2006 alitangazwa bingwa wa dunia wa WBA.
Hata hivyo alikomeshwa na Floyd Mayweather Jr mnamo mwezi Disemba 2007 na Manny Pacquiao mwezi Mei mwaka wa 2009.
BBC

SEBASTIAN VERON AKACHA KUTUNDIKA MADALUGA, ASAINI ESTUDIANTES

Mkongwe wa Man United aliyeahirisha kustaafu soka na kusaini kucheza bure

Ni miaka miwili imepita toka kiungo wa zamani wa Man United na timu ya taifa ya Argentina Juan Sebastian Veron atangaze kustaafu kucheza soka la ushindani, Veron alitangaza kustaafu akiwa na umri wa miaka 39, lakini taarifa zimetoka kuwa staa huyo amerudi kucheza timu ya Estudiantes  ambayo yeye pia ni mwenyekiti na mshahara wake atachangia timu hiyo sawa na kucheza bure.
December 29 2016 taarifa zilizotoka kuhusu kiungo huyo ni kuwa amebadili mawazo hayo ya kustaafu na kuamua kusaini kucheza soka miezi 18, Veron ataonekana dimbani January 8 2017 akiichezea Estudiantes katika mchezo dhidi ya Bayer Leverkusen Florida Cup.
maxresdefault
Veron atacheza mashindano yote ya Ligi na Copa Libertadores lakini kama utakuwa unakumbuka vizuri Veron mwenye umri wa miaka 41, alikuwa ni moja kati ya nyota waliyoiwezesha Man United kuchukua Ligi Kuu England msimu wa 2002-03, Veron alijiunga na Man United 2001 akitokea Lazio kwa uhamisho wa rekodi ya pound milioni 28.1
millardayo

Wednesday, December 28, 2016

AFUKIWA NA JABALI WAKATI AKICHIMBA MAWE AMBONI TANGA



Tanga, MKAZI wa Kongwa Mkoani Dodoma aliefahamika kwa majina ya Thomas Michael (30) amekufa papo hapo baada ya kufukiwa na kifusi wakati akichimba kokoto kijiji cha Mafuriko Amboni Mkoani Tanga.
Tukio hilo lililotokea juzi saa 12 ;30 jioni na kuthibitishwa na kamanda wa polisi Tanga, Benedickt Wakulyamba, baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walisema walisikia mshindo mkubwa  ndani ya machimbo hayo ya kokoto na mawe.
Wakazi hao walisema Michael kwa miaka mingi amekuwa akijishughulisha na uchimbaji wa mawe na kokoto katika machimbo hayo  na amekuwa akiendesha maisha yake kwa kutegemea kuuza mawe na kokoto.
“Nilikuwa narejea nyumbani baada ya kumaliza uchimbaji ng’ambo ya pili ya machimbo haya, nilisikia kishindo kikubwa lakini nikajua maeneo haya ni kawaida tu” alisema Mussa Ally na kuongeza
“Huyu marehemu alikuwa peke yake na ni mtu anaefahamika sana na alikuwa na bidii kwani huchimba mawe hadi wakati mwengine kiza kinaingia ila niseme kuwa  ni ahadi yake imefika” alisema
Ali alisema wachimbaji wengi wa kokoto na mawe katika machimbo hayo ya Mzizima hawana zana za kuchimbia badala yake wamekuwa wakitumia za asili za mitarimbo na nyundo.
Akithibitisha kutokea tukio hilo, kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Benedickt Wakulyamba, alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya Bombo kusubiri familia ya marehemu kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Alisema wakati wa uokozi gari ya kwanza iliyotumwa haikufanikiwa baada ya kuwa na vifaa duni  ambavyo havikuweza kuhimili ufukuzi baada ya jabali hilo kuwa kubwa.
“Kazi utafutaji wa mwili wa marehemu haikuwa kazi rahisi kwani tulidhani ni kifusi cha mchanga bali ni jabali kubwa lililomeguka, tulimaliza kazi ile saa sita usiku na kufanikiwa kuukuta mwili ukiwa umekufa” alisema Wakulyamba
Akitoa wito kwa wachimbaji wa kokoto na mawe katika eneo la machimbo ya Mzizima, kamanda Wakulyamba, aliwataka kuchukua tahadhari kwani miamba hiyo kwa muda mrefu iko na nyufa nyingi.
                                                      



 Wakazi wa kijiji cha Mzizima Amboni Tanga wakiangalia eneo ambalo Thomas Michael alifukiwa na jabali na kufa hapo hapo wakati akichimba mawe.





AMKA NA MAGAZETI NA FREYS TANGA HADI SINGIDA KILA SIKU, LUXURY BUS NA ORDINARY BUS