Bondia Ricky Hatton: Nilijaribu kujiua mara kadhaa
Bingwa wa zamani wa
dunia na bondia wa Uingereza, Ricky Hatton(Kushoto) amefichua kuwa alifikiria
kujiua mara kadhaa kutokana na shinikizo la akili.
Mwanandondi huyo aliyestaafu mwaka wa 2012, ambaye kwa sasa ni mkufunzi wa mabondia, alieleza kuwa amepitia uchungu mwingi."Nilijaribu kujiua mara kadhaa," alisema. "Nilikuwa nikienda kwenye baa, kurudi, nikilia kwenye giza nikiwa nimetoa kisu." "Mwishowe nilihisi kuwa huenda nikajiuwa kwa kulewa kwa sababu nilikuwa na uchungu mwingi".
Hatton ameiambia BBC kuwa kuna umuhimu wa mabondia kupewa ushauri na kusaidiwa wanapostaafu ili kupata nafuu kutoka kwa shinikizo za akili.
"Wanasoka wana maajenti na wasimamizi wanaowasaidia katika vilabu vyao, lakini mabondia, mara tu muda wao unapoisha, unabaki peke yako," alimaliza.
"Kuna mengi yanayofaa kufanywa kuwasaidia mabondia, wengi wetu tanaathirika kwasababu huu mchezo mtu yuko pekee yake na unapostaafu, unaishi maisha ya upweke".
Hatton alipokonywa kibali cha ndondi mwaka wa 2010 baada ya kukiri kutumia mihadarati aina ya 'Cocaine'.
Aidha, ameshinda mapigano 21 yakiwemo kumcharaza bingwa wa dunia wa light-welterweight Kostya Tszyu mjini Manchester mwaka wa 2005 na kuondoka na taji la IBF.
Mwaka wa 2006 alitangazwa bingwa wa dunia wa WBA.
Hata hivyo alikomeshwa na Floyd Mayweather Jr mnamo mwezi Disemba 2007 na Manny Pacquiao mwezi Mei mwaka wa 2009.
BBC
No comments:
Post a Comment