Mkongwe wa Man United aliyeahirisha kustaafu soka na kusaini kucheza bure
Ni miaka miwili imepita toka kiungo wa zamani wa Man United na timu ya taifa ya Argentina Juan Sebastian Veron atangaze kustaafu kucheza soka la ushindani, Veron alitangaza kustaafu akiwa na umri wa miaka 39, lakini taarifa zimetoka kuwa staa huyo amerudi kucheza timu ya Estudiantes ambayo yeye pia ni mwenyekiti na mshahara wake atachangia timu hiyo sawa na kucheza bure.
December 29 2016 taarifa zilizotoka
kuhusu kiungo huyo ni kuwa amebadili mawazo hayo ya kustaafu na kuamua
kusaini kucheza soka miezi 18, Veron ataonekana dimbani January 8 2017 akiichezea Estudiantes katika mchezo dhidi ya Bayer Leverkusen Florida Cup.
Veron atacheza mashindano yote ya Ligi na Copa Libertadores lakini kama utakuwa unakumbuka vizuri Veron mwenye umri wa miaka 41, alikuwa ni moja kati ya nyota waliyoiwezesha Man United kuchukua Ligi Kuu England msimu wa 2002-03, Veron alijiunga na Man United 2001 akitokea Lazio kwa uhamisho wa rekodi ya pound milioni 28.1
millardayo
No comments:
Post a Comment