Mume alikosa kitoweo cha Kuku siku ya Christmas… Kilichofuatia ni ukatili kwa mkewe
Story hii ya kusikitisha inatoka Kenya ambapo jamaa mmoja Daniel Imonje,
alimpiga mke wake kwa shoka mpaka kufariki, majirani walioshuhudia
wakisema eti kisa ilikuwa ni kitendo cha mke wake huyo kutomuandalia
mume wake nyama ya kuku siku ya Christmas, badala yake akaandaa rosti ya
nyama ya ng’ombe.
Ni wengi waliolaani kitendo hicho
kilichotokea Kijiji cha Shanderema, Kenya na mashuhuda wamesema Daniel
alifanya unyama huo akiwa amelewa.
Mtuhumiwa anashikiliwa katika kituo cha Polisi cha Kakamega baada ya kufanya mauaji hayo kwa ajili ya uchunguzi.
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,kumekucha blog
No comments:
Post a Comment