Miezi tisa hakuna majibu ya ndege ya Malaysia Airlines 370, nyingine imepotea leo…
Bado Dunia imebaki njia panda juu ya wapi ilipo ndege ya Malaysia Airlines 370
ambayo ilikuwa na abiria 239, ilipotea miezi zaidi ya nane iliyopita
ikitokea Malaysia kwenda China, ndege nyingine imepotea, ilitokea
Singapore kwenda Indonesia.
Iliyopotea saa chache zilizopita ni AirAsia qz 8501, ilikuwa
na abiria 162 wengi wao walikuwa raia wa Indonesia na Uingereza
imethibitisha kuwa kuna mtu mmoja raia wa nchi hiyo alikuwa akisafiri na
mtoto wake.
Ndege ilipotea wakati rubani
alipolazimika kubadili mwelekeo wa ndege hiyo pasipo kuomba mwelekeo
kutoka kwa waongozaji kutokana na hali mbaya ya hewa.
Ndugu, jamaa na marafiki wa watu waliokuwa wakisafiri kwa ndege hiyo wamejikusanya katika uwanja wa ndege wa Surabaya Indonesia, wakisubiri kupata taarifa yoyote itakayokuwa na matumaini kwao.
Baadhi ya vikosi vinavyotafuta ndege hiyo vimesitisha zoezi hilo kutokana na hali mbaya ya hewa huku vingine vikiendelea.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia, kumekucha blog
No comments:
Post a Comment