Shughuli ya kutafuta ndege ya AirAsia ambayo ilipotea jana Jumapili imeendelea leo tena baada ya kusitishwa kwa muda.
Watu 162
walikuwa kwenye ndege hiyo wakati ikipoteza mawasiliano na kituo cha
kuelekeza safari za ndege. Ndege hiyo ilikuwa safarini kwenda nchini
Singapore ikitokea mji wa Surubaya nchini Indonesia. Shughuli za
kuitafua zinafanyika kwenye kisiwa cha Belitung.
Ndege za
kijeshi kutoka indonesia na singapore zilikuwa zikiisaka ndege hiyo
kusini magharibi mwa pwani ya Borneo ambapo ndege hiyo ilitoweka.
No comments:
Post a Comment