Kumekucha blog
Tanga,JESHI la polisi Tanga, limesema
litaendesha msako kukomesha biashara ya ngono inayoendeshwa katika majumba ya
sterehe pamoja na mitaa inayojulikana kwa kujiuza.
Ujio huo
umekuja baada ya malalamiko ya muda mrefu ya wakaazi wa maeneo ya
Centrol na Ngamiani kati kuongezeka kwa biashara ya kujiuza nyakati za usiku
jambo ambalo linatishia jamii kumomonyoka kimaadili.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na mwandishi wa
gazeti hili jana, kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga, Freisser Kashai, alisema kwa
muda mrefu taarifa za kuwepo kwa biashara ya kujiuza wako nayo na hivyo
wanajipanga kuikomesha.
Alisema kitendo kibaya zaidi ya kuongezeka kwa
biashara ya kujiuza miili ni kuingiliwa na watoto wenye umri mdogo ambao wengi
miongoni mwao ni wanafunzi ambao
hutoroka katika mabweni.
“Kwa muda mrefu tumekuwa katika uchunguzi wa jambo
hili na tumewakamata wengi lakini tukabaini kuwa ni mtandao mpana----hivyo
tukarudi nyuma kujipanga zaidi” alisema Kashai
“Nadhani wewe umekuja wakati muafaka wa suala hili
kwani liko jikoni na limeshachemka---tutakavyoanza operesheni ni siri ya polisi
ila nikuambie biashara ya kujiuza nitaikomesha” alisema
Alisema polisi iko na taarifa zote za majengo
yanayoendesha biashara hiyo na maeneo ya kujiuzia na itanza wakati wowote
kuendesha uvamizi mfululizo hadi kukomeshwa ikiwa na pamoja na kuwapeleka
mahakamani.
Alisema awali waliweza kuikomesha biashara hiyo lakini
baada ya polisi kuacha misako waliweza kurejea tena na kudai kuwa ni kwa kasi
hivyo kutaka kurejea kwa nguvu mfululizo na kuikomesha kabisa.
Kwa upande wa usalama wa raia na mali zao, kamanda
Kashai, aliwataka wananchi kuelekea mwaka mpya kushirikiana na jeshi hilo kwa
kutoa taarifa za matukio na watu ambao watakuwa na mashaka nao.
“Kila mara tumekuwa na utaratibu wa kufanya mikutano
na wananchi mitaani kuwaelimisha mashirikiano na polisi kwa kupeana taarifa za
kihalifu na usalama---hii imesaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza matukio ya
kihalifu” alisema Kashai
Alisema utaratibu wa kufanya mikutano na kujumuika na
wananchi kumelifanya jeshi hilo kuwa karibu na wananchi pamoja na kurahisisha
mawasiliano jambo ambalo limetokomeza matukio ya kihalifu ambayo yalikuwa
kikwazo kwa maendeo.
No comments:
Post a Comment