Alichokisema msimamizi wa Mashtaka Kisutu na shuhuda wa tukio la mtuhumiwa aliyepigwa risasiMitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya Habari leo viliripoti kuhusu mtu mmoja raia wa Sierra Leone, Abdul Koroma ambaye alikuwa anashikiliwa na Jeshi la Magereza nchini kufariki dunia leo Dar baada ya kupigwa risasi na askari Magereza wakati akijaribu kutoroka.
Mtu huyo alifikishwa Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu kwa mara ya kwanza mwaka 2013 kwa tuhuma za kukutwa na dawa
za kulevya na kushitakiwa.
Ameuawa katika uzio wa Mahakama hiyo
baada ya kumtoroka askari magereza aliyekuwa amemsindikiza kujisaidia
ambapo alijaribu kuruka ukuta wa mahakama hiyo.
Shuhuda mmoja wa tukio hilo amesema; “alikimbilia
kwenye ule ukuta pale, akapandisha mpaka pale juu… anataka arukie
upande wa pili magereza washatokea, wakaona hawawezi kukimbia yuko mbali
ndio wakampiga zile risasi kama tatu hivi ndio akafariki…”
Akizungumzia tukio hilo Msimamizi wa Mashtaka Mahakama ya Kisutu Tumaini Kweka amesema; “Wakati wapo kwenye sero ndipo yeye akajaribu kutoroka kwa kujaribu kuruka ule ukuta wetu wa Mahakama ndipo wanausalama wetu ambao wako hapa wakaweza kundhibiti…“
No comments:
Post a Comment