ALIETAKA KUMUUWA PAPA JOHN PAUL AZURU KABURI LAKE
Mehmet Ali Agca aliyetaka kumuua papa John wa Pili mwaka 1981.
Mwanamme mmoja raia wa Uturuki aliyempiga risasi na nusura amuue
aliyekuwa kiongozi wa kanisa katoliki papa John Paul wa pili mwaka 1981
ameweka maua kwenye kaburi lake katika makao makuu ya kanisa katoliki ya
Vatican.
Ziara ya Mehmet Ali Agca kwenye makao ya Vatican inafanyika miaka 30
tangu John Paul amtembelee gerezani na kumsamehe kwa kujaribu kumuua.
Bwana Agca aliomba kukutana na kiongozi wa sasa wa kanisa katoliki papa Francis lakini hata hivyo ombi lake lilikataliwa
Aliachiliwa kutoka gerezani nchini Italia mwaka 2000 na kisha baadaye
akatumikia kifungo chengine cha miaka 10 nchini Uturuki kwa makosa
tofauti.
Hadi sasa sababu zake za kutaka kumuua papa John Paul hazijulikani.
No comments:
Post a Comment