Unafahamu jezi inayoongoza kwa ufungaji wa magoli mengi England? Rekodi iko hapa…
Katika hali ya kawaida namba
zinazoandikwa kwenye jezi za wachezaji wa timu za mchezo wa soka
huwakilisha nafasi wanazocheza uwanjani .
Namba hizi kiasili huendana na eneo
ambalo mchezaji husika anapendelea kucheza kwa mfano jezi namba moja
huvaliwa na kipa , jezi namba tisa huvaliwa na mshambuliaji na kadhalika
na kadhalika.
Utamaduni huu umekuja kubadilika hivi
karibuni ambapo Wachezaji wamekuwa na kawaida ya kuvaa jezi kutokana na
ukaribu walio nao na namba fulani au wakati mwingine sababu za
kihistoria na mazoea pia yamekuwa yakiongoza utamaduni wa kuvaa namba
husika .
Kiutamaduni kuna namba huvaliwa na
wachezaji wa aina fulani, mfano wake ni jezi namba kumi ambayo siku zote
imekuwa ikivaliwa na wachezaji wenye vipaji na ubora kuliko wote na
mara nyingi huwezi kukuta mchezaji wa kawaida anavaa jezi namba kumi.
Hili limeweza kudhihirika msimu huu
kwenye ligi ya England ambako wachezaji wanaovaa jezi namba 10
wameongoza kwa kung’aa hasa kwenye ufungaji wa mabao muhimu.
Takwimu zinaonyesha kuwa kati ya mabao
457 ambayo yamefungwa hadi sasa kwenye mechi za ligi kuu ya England
mabao 56 yamefungwa na wachezaji wanaovalia jezi hii ambayo siku zote
inahusishwa na ‘mafundi’ wa mpira.
Idadi ya mabao yaliyofungwa na wachezaji
wanaovaa jezi namba 10 kwa ujumla ndio idadi kubwa ya mabao kufungwa
na wachezaji wanaovaa namba zote ikifuatiwa na namba 9 ambao wachezaji
wake wamefunga jumla ya mabao 38 ikiwa ni tofauti ya mabao 18 kati ya
wachezaji wanaovaa jezi namba 9 na namba 10.
Katika kundi la wachezaji wanaovaa namba 10 wako nyota kama Eden Hazard, Wayne Rooney, Wilfred Bony, Jack Wilshere na Romelu Lukaku huku Bony na Rooney wakiongoza orodha hiyo wakiwa wamefunga mabao 8.
Wafungaji Bora kuendana na namba za Jezi
1. Jezi namba 10 – Magoli 56
2. Jezi namba 9 – Magoli 38
3. Jezi namba 18 – Magoli 33
4. Jezi namba 19 – Magoli 32
5. Jezi namba 23 – Magoli 24
6. Jezi namba 11 – Magoli 23
6. Jezi namba 16 – Magoli 23
6. Jezi namba 17 – Magoli 23
7. Jezi namba 15 – Magoli 22
8. Jezi namba 21 – Magoli 19
*Takwimu hizi ni kwa msimu huu pekee.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,kuekucha blog
No comments:
Post a Comment