Utafiti kuhusu athari za chumvi kwenye chakula .
Moja ya vitu ambavyo vimekuwa muhimu kwenye chakula cha mwanadamu ni chumvi ambayo hutumika kuongeza ladha ya chakula ambacho hutumika mezani . Umuhimu wa kiungo hiki umefikia hatua ya waswahili kuibatiza chumvi jina la utani ambalo ni Mkuu Wa Jiko .
Hata hivyo chumvi inaweza kuwa na madhara pale ambapo inatumika kuliko kawaida na madhara hayo ni kwa afya ya mtumiaji .
Je chumvi ni mbaya kwa Afya yako?
Mwili wa mwanadamu unahitaji chumvi kwa kiwango Fulani kwani inasaidia kuongeza mnadini ambayo mwili wako unayahitaji . Hatari ni pale unapokula chumvi nyingi kuliko kiwango ambacho mwili wako unahitaji . Imagundulika kuwa chumvi husababisha matatizo ya shinikioz la damu hali ambayo inaweza ikaongeza uwezekano wa mtu kupata matatizo ya shambulio la moyo pamoja na hatari nyingine za magonjwa ya moyo . Madaktari wanashauri utumiaji wa chumvi kwa kiwango cha chini ili kuepukana na matatizo haya .
Je kiasi gani cha chumvi kinazidi kiwango cha kawaida .
Kimsingi hupaswi kula zaidi ya gramu tano za chumvi kwa siku , hii ni sawa na kijiko kimoja cha chai ambacho kina ujazo wa milligram 5 . Kiwango hiki kinajumuisha chumvi ambayo unaongeza ukiwa unapika jikoni , chumvi unayoongeza mezani wakati wa kula na ile chumvi ambayo inapatikana kwneye chakula kiasili hii ni kwa sababu kuna vyakula ambavyo ndani yake kuna chumvi hata kama havina ladha ya chumvi . Mfano wa vyakula ambavyo tayari vina chumvi ndani yake ni Mikate , Sausage na nyama za kusaga , supu ya kutengenezwa kiwandani , vyakula vya nafaka ambavyo hutumika kwenye kifungua kinywa (breakfast) n ahata baadhi ya biskuti .
Je tunatumia chumvi nyingi kuliko kawaida ?
Waafrika wengi huwa na kasumba ya utumiaji wa chumvi kwa kiwango kikubwa kuliko kawaida na hii imezoeleka sana kuanzia majumbani mpaka mahotelini .
Ni rahisi sana kutumia chumvi nyingi kuliko kawaida wakati wa milo ya kila siku .
Nusu ya chumvi ambayo hutumiwa na watu ni chumvi inayopatikana kwenye vyakula hasa vile vya kutengenezwa viwandani ambayo huwekwa wakati wa utengenezaji wa vyakula hivi huko huko viwandani ili kuvifanya vikae kwa muda mrefu .
Nusu nyingine ni ile ambayo ambayo huongezwa jikoni na ile ambayo watu huongeza mezani wakati wa kula ili kukoleza ladha ya chakula husika .
Nini kinatengeneza chumvi
Chumvi inatengenezwa na vitu viwili ambavyo ni sodium na chloride , Sodium ni sehemu ya chumvi ambayo ambayo huongeza presha ya damu au kwa lugha inayoeleweka zaidi huongeza shinikizo au msukumo wa damu hasa pale unapotumia chumvi nyingi kuliko kiwango cha kawaida . Pamoja na ukweli kwamba tunatumia chumvi nyumbani , taarifa zinaoandikwa kwenye vihifadhi vya vyakula hasa vile ambavyo vinatengenezwa viwandani huonyesha kiwango cha madini ya sodium ambayo yametumika kwenye chumvi . Kijiko kimoja cha chai mara nyingi huwa kina miligramu 2000 za sodium .
Ni jinsi gani tunaweza kutumia kiwango cha chini cha chumvi kwenye vyakula ?
Haiwezekani kupunguza kiwango cha chumvi ndani ya siku moja au ghafla , mabadiliko yanapaswa kufanyika hatua moja baada ya nyingine .
Muhimu ni kujizoesha hisia ya kudhani kuwa chakula kina ladha hata pale ambapo chumvi haijakolea
Kama una kawaida ya kuongeza chumvi nyingi mezani hatua ya kwanza ni kuondoa kile kikopo kidogo cha chumvi mezani hasa wakati wa chakula , hii ni kwa sababu unapaswa kukumbuka kuwa kama ulishaongeza chumvi tangu jikoni hauna sababu ya kuongeza nyingine mezani .
Jaribu pia kupunguza kiwango cha chumvi unachoongeza wakati wa mapishi yako , unapswa kuonja wakati ukiwa unapika ili kuepuka kuongeza kiwango cha chumvi ambcho kinaweza kuwa hatari kwa Afya yako . Kama chakula chako kina viungo ambavyo ndani yake kuna chumvi ya asili hupaswi kuongeza chumvi nyingine juu yake .
Katika tafiti zilizofanyika hivi karibuni imefahamika kuwa kuna baadhi ya vitu vinavyoweza kutumika kama chuimvi ambavyo havna madhara sawa na ya chumvi kwenye mwili wa mwanadamu na mojawapo ni limao pamoja na ndimu .
Kiungo kingine kinachoweza kuchukua nafasi ya chumvi kwenye chakula chako ni mdalasini .
Vyakula visivyo na chumvi nyingi?
Vyakula ambavyo havijatengenezwa kiwandani kwa maana ya vyakula halisi mara nyingi huwa havina chumvi nyingi na hii inamaanisha kuwa unapaswa kuchagua vyakula vya asili kuliko vile ambavyo vimetengenezwa viwandani .
No comments:
Post a Comment