Jumamosi December 27, story sita kubwa kutoka kwenye Magazeti ya leo T’zania
Mtu mmoja amewafyatulia risasi watu
wawili na kupelekea mmoja kufariki na mwingine kujeruhiwa akiwalalamikia
kumpigia kelele wakati watu hao walipokuwa kwenye mkesha wa harusi Dar.
Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kipolisi
Ilala, David Mwambunga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo japo
amekataa kuzungumzia suala hilo kwa kuwa yeye sio msemaji rasmi.
Majeruhi wa tukio hilo, Goodluck
Madaraka amesema siku ya tukio walikuwa wakicheza muziki majira ya saa
tano usiku ndipo jirani yao Lucas Muhabe alitoka na panga akiwafukuza
kwamba wanampigia kelele, muda mfupi baadaye akarudi na bastola na
kuanza kupiga risasi hewani ambapo moja ilimpata mpita njia Mahamudu
Muhasi kichwani, akafariki.
Kaka wa marehemu amesema mdogo wake alikuwa akipita njia tu jirani na ilipo sherehe hiyo hivyo ameuawa lakini hakuhusika.
NIPASHE
Kuongezeka kwa ndoa za mikeka
kumesababisha kuongezeka kwa talaka katika Mahakama Kuu Z’bar ambapo
mwanaharakati wa Chama cha Wanahabari, Amina Talib amesema ndoa hizo
ambazo zinafahamika pia kama ndoa za kukamatiwa zinaharibu mfumo mzima
wa maisha.
Amina alisema katika Ripoti zilizotolewa
na chama hicho, Mahakama za kadhi ambazo zimekuwa na majukumu ya
kusikiliza kesi za ndoa na mirathi zimeelemewa na idadi kubwa ya maombi
ya talaka huku watendaji wa Mahakama hiyo wakilaumu wananchi kutochukua
hatua yoyote kunusuru hali hiyo.
Wazazi wametakiwa kuwalea watoto wao kwa
maadili ili kukwepa vitendo vya ushawishi wa kuingia katika uhusiano wa
kimapenzi kabla ya umri.
HABARI LEO
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Mary
Nzuki amesema wanamshikilia mfanyabiashara Lucas Sasha kwa kosa la
kumuua mpita njia Mahmoud Ally kwa kumpiga risasi maeneo ya Tabata
Kisukulu wakati wa sherehe za Christmas.
Kwa mujibu wa maelezo aliyoyatoa Sasha
amesema kuwa kulikuwa na kundi kubwa la vijana waliokuwa wanapita mbele
ya nyumba yake hivyo akadhani kuwa amevamiwa na vibaka, akaamua kupiga
risasi.
Kamanda Nzuki amesema mfanyabiashara
huyo anamiliki bastola hiyo kihalali, kwa sasa Polisi wanamshikilia kwa
ajili ya uchunguzi wa tukio hilo
JAMBO LEO
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Nishati na Madini, Victor Mwambalaswa amesema kuwa yupo tayari
kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti wa Kamati hiyo kwa kuwa anatambua
maana ya uwajibikaji.
Mwambalaswa amesema anayaheshimu
maazimio ya Bunge hivyo ni lazima akubaliane nayo kwa kuwa yeye alikuwa
mmoja ya waliopitisha maazimio hayo.
Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya
Naibu Spika Job Ndugai kutoa tamko kwamba washukiwa wote wa sakata la
uchotwaji wa pesa za Escrow wahakikishe wanaachia ngazi wiki mbili kabla
ya Kikao cha Bunge kuanza hapo Januari 27.
TANZANIA DAIMA
Mtu mmoja asiyefahamika amekufa kwa
kujilipua bomu alilokuwa amelenga kuwalipua Polisi waliokuwa katika
doria Songea siku ya Krismasi.
Kaimu Mkurugenzi wa makosa ya jinai
nchini, Naibu Kamishna Diwani Athumani amesema tukio hilo lilitokea juzi
Desemba 25 majira ya saa moja usiku ambapo Polisi walipitwa na gari
dogo ambalo liliegeshwa mbele yao na muda mfupi wakasikia kishindo cha
mlipuko.
Watu kadhaa walionekana wakiuchukua
mwili wa mtu huyo aliyejeruhiwa ili waupakie kwenye gari iliyokuwa
imesimama mbele ya gari ya Polisi, baada ya kuwaona Polisi waliuacha
mwili wa mtu huyo na kukimbia.
Katika tukio hilo Polisi wawili
walijeruhiwa lakini hali zao zinaendelea vizuri huku upelelezi
ukiendelea kubaini wahusika wa tukio pamoja na lengo lao kwa kuwa
mazingira yanaonyesha kuwa lengo lilikuwa kuwadhuru Askari Polisi hao
waliokuwa doria.
TANZANIA DAIMA
Wengi tumezoea kwamba kila anayehudhuria sherehe kubwa za Kitaifa na kupita red carpet lazima awe amevalia vizuri kuendana na sherehe husika.
Story ni kwamba mama mzazi wa Naibu Rais
wa Kenya, William Ruto ambaye jina lake Sarah Cheruiyot alihudhuria
siku ya sherehe za maadhimisho ya Uhuru wa Kenya akiwa amevaa ndala au
wengine huyaita malapa na akapita zake red carpet.
Story ni kama ilikuwa kubwa uwanja wa
Nyayo ambapo sherehe za maadhimisho hayo zilifanyika, lakini wengine
wanahisi kwamba huenda mama huyo alifanya hivyo kama njia ya kutangaza
bidhaa hiyo.
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,kumekucha blog
No comments:
Post a Comment