TAARIFA ZA AWALI MWANZO KUHUSU NDEGE YA AIRASIA QZ8501 YAPOTEA IKIWA NA WATU 162 LEO ASUBUHI
Ndege ya AirAsia, QZ8501 iliyokuwa na watu 162 ikitokea Indonesia
kwenda Singapore iliyopoteza mawasiliano jana asubuhi.Ndugu, jamaa na
marafiki wa abiria waliokuwa kwenye ndege ya AirAsia QZ8501 wakiwa na
majonzi wakati wakisubiri taarifa kuhusu ndugu zao katika Uwanja wa
Ndege wa Surabaya, Indonesia.
Kati ya watu hao 162, abiria walikuwa 155, marubani 2 na wafanyakazi
wa ndege hiyo 5. Watu 157 ni raia wa Indonesia, 3 raia wa Korea Kusini, 1
kutoka Malaysia na 1 raia wa Singapore.
Imeelezwa kuwa kabla ya ndege hiyo kupoteza mawasiliano, rubani
aliomba kubadili uelekeo wa kawaida kutokana na hali mbaya ya hewa.
Ndege hiyo ilifanyiwa matengenezo kwa mara ya mwisho Novemba 16, 2014
kama ilivyokuwa imepangwa.
Rubani wa ndege hiyo ana uzoefu wa saa 6,100 angani huku msaidizi wake akiwa na uzoefu wa saa 2,275.
Miongoni mwa abiria 155 waliokuwa kwenye ndege hiyo, 138 ni watu wazima, 16 watoto na 1 mama mjamzito. hapa jamaa na warafikiwa ndugu wakinakili majina ya abiri waliopotea
QZ8501 imetoka Indonesia saa 11: 27 alfajiri na ilitarajiwa kuwasili Singapore saa 2:37 asubuhi.
Msemaji wa wizara ya usafiri nchini Indonesia amesema mawasiliano yalipotea kati ya visiwa vya Kalimantan na Java.
Wataalamu wa safari za ndege wanasema kuwa huenda ndege hiyo iliishiwa na mafuta
No comments:
Post a Comment