Kumekucha blog
Same,MKUU wa Wilaya ya Same, Herman
Kapufi, amewataka wakazi wanaokaa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi kuacha
kushirikiana na majangili na badala yake wawafichue vyenginevyo atakaebainika
kufanya hivyo atafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mheza kata ya
Maore wakati wa kukabidhi mradi wa jengo la wodi ya mama na mtoto lililojengwa
na Hifadhi ya Taifa Mkomazi(Tanapa), Kapufi amesema Serikali imejipanga
kukabiliana na ujangili ndani ya hifadhi hiyo.
Amedai kuwa ziko taarifa za baadhi ya watu kuwahifadhi
na kuficha taarifa za majangili ndani ya hifadhi hiyo na hivyo kuwataka kuacha
kufanya mara moja vyenginevyo wanaweza
kujikuta wakikabilia na mkono wa sheria.
“Ndugu zangu munaokaa ndani na nje ya hifadhi ya
taifa ya Mkomazi tuache kuwalinda majangili wanaotumalizia rasilimali
zetu----tukiwalinda watatumalizia vivutio vyetu na watalii hawatakuja na
tutakaoathirika ni sisi” alisema Kapufi
“Hifadhi ni ya kwenu ninyi wenyewe na matunda yake ni
kama haya ya leo---kama sio hifadhi ya taifa mkomazi jambo hilo lisingekuwepo
na taarifa nilizonazo ni kuwa kuna mengi wamewafanyia” alisema
Akizungumzia baadhi ya watu kuchimba madini na kukata
miti ndani ya hifadhi hiyo, Mkuu huyo wa Wilaya amekemea vikali na kusema
Serikali imejipanga kukabiliana na jambo hilo na kuwataka kuacha mara moja.
Alisema vitendo
hivyo vinachangia kuwakimbiza wanyama na mvua kunyesha na kusema kuwa
hakikubaliki na operesheni ya kulikomesha jambo hilo litaanza mara moja ikiwa ni
kuzilinda rasilimali za nchi.
Awali akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkuu wa
Hifadhi ya Taifa Mkomazi, Donat Mnyagatwa, alisema mradi huo hadi kukamilika
kwake umegharimu zaidi ya shilingi milioni 81 ikiwa wananchi wamechangia
milioni 24.
Alisema mradi wa jengo la wodi ya mama na mtoto
limekuja baada ya hifadhi hiyo kuona kero wanayoipata wakazi wa vijiji vya
Mheza na Maore pamoja na vijiji jirani.
“Sisi Mkomazi baada ya kuona kero ya wananchi
wanayoipata wenzetu mama wajawazito tukaona ni vyema tutawapunguzia usumbufu wa
kufuata huduma masafa marefu kwa kujenga kituo hapa Maore” alisema Kapufi
Alisema
mradi wa jengo hilo litakuwa msaada mkubwa kwa
wakazi hao na vijiji vya jirani kwani kwa muda mrefu walikuwa katika
adha na mateso na hivyo kuwataka kulitunza ili kuwa mkombozi kwa mama
wajawazito na
watoto.
No comments:
Post a Comment