NHC yakabiliana na tatizo la moyo nchini kwa kusaidia matibabu ya watoto 53 nchini India
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa
hafla fupi iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam ya kuwaaga jumla ya watoto 55 wenye matatizo ya
ugonjwa wa Moyo kati ya 104, waliofadhiliwa na Lions Club ya jijini, kwa
ajili ya kwenda kutibiwa nchini India. Watoto hao 55 wa awamu ya kwanza
wanaanza kuondoka nchini leo.
Rais wa Lions (Host) Club ya Dar
es Salaam, Mathew Levi, akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwaaga
watoto 55 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo kati ya 104, kwa ajili ya
kwenda kutibiwa nchini India. Watoto hao 55 wa awamu ya kwanza wanaanza
kuondoka nchini leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akivishwa Beji ya
miaka 50 ya Lions Club na Makamu wa Gavana wa Club hiyo, kwa nchi za
Tanzania na Uganda, Hyderali Gangji, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga
watoto wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo wanaokwenda nchini India
kutibiwa. Hafla hiyo ilifanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya
Serena jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na
Makamu wa Gavana wa Club
hiyo, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watoto 55 wenye matatizo ya
ugonjwa wa Moyo kati ya 104, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India.
Watoto hao 55 wa awamu ya kwanza wanaanza kuondoka nchini leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa
hafla fupi iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam ya kuwaaga jumla ya watoto 55 wenye matatizo ya
ugonjwa wa Moyo kati ya 104, waliofadhiliwa na Lions Club ya jijini, kwa
ajili ya kwenda kutibiwa nchini India. Watoto hao 55 wa awamu ya kwanza
wanaanza kuondoka nchini leo.
Badhi ya watoto hao wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo, wakiwa na mama zao wakati wa hafla hiyo.
Badhi ya watoto hao wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo, wakiwa na mama zao wakati wa hafla hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi
mtoto, Nabil Hahya (4) kutoka Jijini Dar es Salaam, mmoja kati ya watoto
55 wa awamu ya kwanza kati ya 104 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo
wanaokwenda kutibiwa nchini India, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga
watoto hao iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena
Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mama wa motto huyo, Amina Yahya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiinua glasi juu
kumtakia heri Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na
baadhi ya wadau wa Lions Club, baada ya hafla fupi ya kuwaaga watoto
hao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya wadau wa Lions Club, baada ya hafla fupi ya kuwaaga
watoto hao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya wadau wa Lions Club, baada ya hafla fupi ya kuwaaga
watoto hao.
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
limechangia kiasi cha takribani shilingi milioni 29 katika kuokoa maisha
ya watoto wenye maradhi mbalimbali ya moyo nchini ambao wanaondoka leo
kwenda India kwa upasuaji. Watoto hao 53 wameagwa na Makamu wa Rais, Dk.
Mohammed Gharib Bilal.
Akizungumza na wazazi wa watoto
hao waliofika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo Dk Bilal
alililipongeza Shirika la Nyumba la Taifa pamoja na wadau mbalimbali
waliojitolea kuhakikisha wanakabiliana na tatizo la moyo ambalo
linaongezeka kwa kasi.
“Kama Serikali hatuwezi
kukabiliana na tatizo hili peke yetu hivyo nawapongeza wadau mbalimbali
binafsi na taasisi zilizojitolea kwaaajili ya kuokoa maisha ya
Watanzania wenzao, ni jambo linalotia faraja na ni desturi ya Watanzania
kusaidiana,”alisema.
Alisema Serikali inaendelea na
jitihada mbalimbali za kukabiliana na tatizo hilo ikiwa ni pamoja na
kujenga taasisi za kukabiliana na tatizo hilo nchini ili kusudi hudma
ziweze kuwafikia Watandania wengi zaidi.
Naye Mratibu wa magonjwa ya moyo
katika Klabu ya Lions ya Dar es Salaam, Dk. Rajni Kanabar, alisema
wagonjwa hao watatibiwa katika hospitali mbalimbali nchini India.
Alisema safari ya wagonjwa hao
imeratibiwa kwa pamoja na Klabu ya Lions ya Dar-es-Salaam (Host),
Regency Medical Centre na Wizara ya Afya ya Zanzibar.
Alisema katika kundi hilo,
watakuwamo wauguzi wawili na madaktari wawili na wanatarajiwa kurudi
nyumbani baada ya wiki nne zijazo.
Dk. Kanabar alisema wagonjwa 15
watatibiwa katika hospitali ya Jaypee Health Care Heart Institute
iliyoko mji wa New Delhi na wengine 27 watatibiwa katika taasisi kubwa
ya Fortis Escorts Heart iliyoko New Delhi, India.
“Watafanyiwa upasuaji ambao
utagharimu Dola 2,500 za Marekani kwa kila mgonjwa na watapewa Dola
500 kwa ajili ya kujikimu wakiwa huko,” alisema Dk. Kanabar ambaye pia
ni Mwenyekiti wa Hospitali ya Regency Medical Centre.
Alisema hospitali ya Escorts ni
miongoni mwa hospitali kubwa duniani kwa matibabu ya moyo na imekuwa
ikiwafanyia upasuaji wagonjwa wa moyo kutoka Tanzania kwa punguzo kubwa
la gharama za matibabu hayo.
Aliishukuru Wizara ya Afya ya
Zanzibar kwa kuchangia nauli za ndege kwa wagonjwa 33 na kutoa Dola 500
kwa kila mgonjwa na Ubalozi wa India ambao viza za bure kwa wagonjwa
wote kupitia balozi wa nchi hiyo hapa nchini, Debnath Shaw.
Dk. Kanabar aliwataja wengine
waliochangia kuwa ni Bank M iliyochangia Dola 10,000 gharama za
upasuaji wa wagonjwa wanne, Shirika la Nyumba la Taifa limechangia
shilingi milioni 29
na Klabu ya Lions Dar es Salaam
(Host) Dola 16,500, Pradeep Kumar wa Bengaluru, India Dola 16,400,
Regency Medical Centre Dola 12,500, wanafunzi wa British Columbia
University Vancouver, Canada na Jumuiya ya Theosophical ya Dar es
Salaam Dola 10,000.
Wengine ni Riyaz Hassan Ali wa
Karim Foundation Marekani Dola 9,000, Familia ya Mohamed Gulam Dewji
Dola 5,000, Africarriers Dola 5,000, Lakhan Pal wa Dar es Salaam Dola
2,500, Nashrin Sarkai wa Marekani Dola 5,000, Hazi Abbas wa Dar es
Salaam Dola 2,500, Lion Siraz Jessa wa Dar es Salaam Dola 2,500, Lion
Mohamed Laljee, Lion Yusuf Dalal, Lion Karim Meetha, Lion Nazmu Dola
3,500, Guru Sikh Sabha wa Dar es Salaam Dola 5,000, Harun Zacharia,
Salim Turkey Dola 5,000, Dk. Kiran Nad Pallavi Patel wa Global
Foundation Marekani Dola 10,000, Habib African Bank ya Dar es Salaam
Dola 3,000 na Prem Kapoor & Family ya Mwanza Dola 3,000 na
Gavana wa District 411B.
No comments:
Post a Comment