Kwenye rekodi za mauzo ya filamu za Sony, hii imevunja rekodi ndani ya siku tano tu!
Labda nikupe dondoo kidogo kuhusu movie
hii, story ilianzia November 22 ambapo system ya computer za Kampuni ya
Sony zilivamiwa na watu wasiofahamika na kuvujisha taarifa mbalimbali za
siri ikiwemo email za mastaa mbalimbali Duniani, mishahara yao na
baadhi ya script za movie zitakazotolewa siku za karibuni.
Movie ya ‘The Interview’
ilivuja pia, story ya movie hii iko hivi; waandishi wawili wa Habari
walipata mwaliko kuonana na Rais wa Korea Kaskazini, wanapanga njama na
CIA ili wamuue Rais huyo, Kim Jong-un.
Serikali ya Marekani ililaani kitendo
cha uvamizi huo kwa kuishutumu Serikali ya Korea Kaskazini kwamba
imehusika na uvamizi wa system hiyo, Korea walikanusha huku kikundi cha
waliohusika kikipiga mkwara wa kushambulia kumbi zote za sinema Marekani
ambako ilipangwa kuonyeshwa movie hiyo, Rais Obama akasema ionyeshwe na hakuna hatari yoyote ya mashambulizi itakayotokea.
Baada ya mvutano huo, siku ya Christmas
December 25 iliachiwa rasmi mtandaoni ambapo watu walikuwa na uwezo wa
kuidowload na kutazama katika kumbi mbalimbali ilikokuwa ikionyeshwa.
Baada ya kuanza kuuzwa movie hiyo, Sony
wamesema ndani ya siku tatu movie hiyo imefanya mauzo ambayo haikuwahi
kutokea siku za nyuma, imeuza zaidi ya dola mil. 18 ndani ya siku tatu,
hii ni rekodi ya kipekee haikuwahi kutokea mauzo ya kiasi hiki siku za
nyuma.
Hapa kuna trailer ya movie hiyo, unaweza kuitazama mtu wangu.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,kumekucha blog
No comments:
Post a Comment