Wakati wengine wakisherehekea kupata watoto…hali si shwari kwenye ndoa ya mchekeshaji maarufu Chris Rock

Mchekeshaji
maarufu nchini Marekani Chris Rock ameamua kuachana na mpenzi wake wa
siku nyingi Malaak Campton baada ya kudumu nae kwenye ndoa kwa miaka 19.
Katika maelezo yaliyotolewa na mkewe Malaak alisema “baada ya
mgongano mrefu na kudumu kwa miaka 19 katika ndoa yetu,Chris na mimi
tumeamua kutengana na kila mmoja kufanya mambo yake”.

Mwanasheria
wa mchekeshaji huyo Robert S.Cohen alithibitisha kupokea barua ya
talaka toka kwa Kris kwenda kwa mkewe Malaak na kusema haya ni mambo
binafsi na wahusika wameamua kuyafanya kwa usiri ili kulinda heshima ya
watoto wao,”alisema Mwanasheria huyo katika moja ya jarida la nchini
humo.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupiti,kumekucha blog
No comments:
Post a Comment