KOCHA SUPER D AMPIGA TAFU YA VIFAA BONDIA MUSSA CHITEPETE WA SONGEA VIFAA
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ katikati akimkabidhi vifaa bondia Mussa Chitepete wa Songea vilivyotolewa na Super D kwa kushilikiana na marafiki zake wa kwenye mtandao wengine kulia ni Kiliani Shayo na Rajabu Mkamba ambaye ni mdau mkubwa wa kuhamasisha kusaidia mchezo wa masumbwi Picha na SUPER D BOXING |
Na Mwandishi Wetu, kumekucha blog
KOCHA wa kimataifa wa mchezo wa
masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ kwa kushilikiana na marafiki
zake wa kwenye mtandao wa kijamii wa watsupp wamemkabidhi vifaa bondia
Mussa Chitepete wa Songea kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa masumwi
nchini
Super D alimkabidhi vifaa hivyo
bondia huyo hivi karibuni alivyotembelea jijini Dar es salaam kuja
kushiliki mchezo wa masumbwi ambapo alipatiwa glove,gum shit,clip
bandeji pamoja na kamba kwa ajili ya kurukia
Vifaa hivyo vilivyotolewa na
super D kwa kushilikiana na mdau mkubwa wa mchezo wa masumbwi nchini
Rajabu Mkumba ambaye ndie mwamasishaji mkubwa katika mtandao huo kwa
ajili ya kusaidia mabondia
Baada ya kukabidhiwa msaada huo bondia Mussa Chitepete wa Songea alishukuru wadau
Mbalimbali kwa kumpatia vifaa na kumpongeza kocha Super D kwa kuanzisha mtandao ambaoumekuwa muhimu sana kwangu kwa mimi kupata vifaa najua sitotumia peke yangu wapo na wenzangu tutakao tumia nao pamoja vifaa hivi ambavyo itakuwa chachu ya kuinua mchezo wa masumbwi Songea
Mbalimbali kwa kumpatia vifaa na kumpongeza kocha Super D kwa kuanzisha mtandao ambaoumekuwa muhimu sana kwangu kwa mimi kupata vifaa najua sitotumia peke yangu wapo na wenzangu tutakao tumia nao pamoja vifaa hivi ambavyo itakuwa chachu ya kuinua mchezo wa masumbwi Songea
Nae mdau mkubwa wa masumbwi
nchini Rajabu Mkamba amesema kwa kushilikiana na Super D wamefanya mambo
mengi kwa ajili ya kuinua mchezo wa masumbwi nchini hivyo atutoishia
hapa tutaendelea kutoa sapoti kwa mabondia na wadau mbalimbali ili
mchezo usonge mbele na wadhamini wajitokeze kusaidia ili vijana wawe na
moyo wa kucheza mchezo wa masumbwi
No comments:
Post a Comment