Rihanna kumtoa kaka yake kwenye ‘Game’.
Siku zote ua huota kwenye bustani ambayo ina maua mengi , msemo huo umeonekana kuwa kweli kwenye familia ya mwanamuziki Robyn Fenty mwenye asili ya visiwa vya Barbados ambaye wengi humfahamu kama Rihanna baada ya mwanadada huyo kuamua kumsaidia ndugu yake wa kiume kuingia rasmi kwneye tasnia ya muziki ambako mwanadada huyo amekuwa akifanya vizuri .
Rihanna ameamua kumsaidia mdogo wake wa kiume ambaye anafahamika kwa jina la Rorrey ‘kutoka’ kwenye Sanaa ya muziki ambako kijana huyo anafanya muziki wa mtindo wa kufoka yaani Hip-Hop.
Rihanna mwenye umri wa miaka 26 aliamua kurudi nyumbani kwao huko visiwani Barbados ambako pamoja na kuwa mapumzikoni amekuwa ‘bize’ kikazi akimsaidia ndugu yake Rorrey Fenty kujaribu kujijengea jina katika muziki kama ilivyokuwa kwake .
Rihanna amekuwa akimshauri ndugu yake huyo kuzingatia muziki na si mambo mengine ambayo hayawezi kumsaidia yakiwemo kuishi mtindo wa maisha wa kuendekeza anasa na starehe .
Chanzo kimoja cha habari hii kimearifu kuwa Rihanna anatambua kuwa kaka yake ana kipaji kama msanii lakini pia anapenda sana maisha ya starehe jambo ambalo linaweza kumfanya ashindwe kuzingatia kazi na kushindwa kufanikiwa .
Rihanna anafahamu kuwa anao uwezo wa kumsaidia ndugu yake kwani akifanya naye wimbo bila ubishi wimbo huo utafanya vizuri na kuwa kama jukwaa la kuanzia kwa ndugu yake mwenye umri wa miaka 23 na ndio maana amemaua kupoteza muda wake kuhakikisha anamsaidia ili kumfanya ‘atoke’ kisanaa kama ilivyokuwa kwake (Rihanna)
Rorrey Fenty anafahamika kwa jina la kisanii la GALLEST na hadi sasa ameshaachia ‘mixtape’ ambayo inafahamika kama ‘Intolerable Cruelty’ ambayo aliiachia mwanzoni mwa mwaka 2014 na Rihanna ana matumaini kuwa atakuwa msaada mkubwa kwa ndugu yake .
Kwa upande wake Rihanna mwenyewe ambaye kwa sasa amekuwa kwenye mapumziko akiwa amesimamisha kazi zake zote za Sanaa atarudi rasmi kwenye Game mapema mwaka 2015 na anatarajiwa kuachia wimbo utakaojulikana kama R8’ ambao ameufanya akishirikiana na msanii Ryan Tedder wa kundi la muziki wa rock la One Republic.
No comments:
Post a Comment