Monday, December 29, 2014

BODABODA AUWAWA KINYAMA KWA KUCHOMEWA NYUMBA AKIWA AMELALA




Kumekucha blog
Tanga,WATU wasiojulikana wamevamia nyumba ya dereva wa bodaboda, Omari Shaban(32) na kumuua kisha kuchoma nyumba yake akiwa amelala kwa kile kilichodaiwa ni visa na wivu wa kimapenzi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo, kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga, Frasser Kashai, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 8 usiku kijiji cha Kireguru kata ya Kwediboma Wilayani Kilindi baada ya watu wasiojulikana kuvamia nyumba na dereva huyo  na kumuuwa.
Alisema uchunguzi wa kipolisi umebaini kuwa dereva huyo alikuwa na ugomvi wa muda mrefu na jamaa ambaye kamanda hakumtaja jina lake kwa madai ya kuchukua bibi wa watu.
“Uchunguzi wetu wa kipolisi umebaini kuwa chanzo cha tukio lile ni mambo ya kimapenzi----alikuwa na mahusiano na bibi wa watu na aliwahi kukanywa kuacha tabia hiyo lakini alikuwa mkaidi” alisema Kashai na kuongeza
“Ila nisema kuwa kitendo ambacho kimefanyika ni cha kikatili na hakikubaliki hivyo tuko katika uchunguzi nani wamefanya jambo hili----mara baada ya kukamilika tutawasaka na kuwafikisha katika vyombo vya sheria” alisema Kashai
Katika tukio jengine , kamanda Kashai alisema polisi Wilayani Handeni inawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kumuua kwa kumnyonga hadi kufa  mwanafunzi wa darsala la sita shule ya Kivesa, Isaka Beda na mwili wake kuutundika juu ya mti.
Aliwataja watu hao kuwa ni,Khalid Ponera(36), Msuya Fransiss(20), Athuman Nassour(20) na Issa Hassan (32) wote wakazi Handeni na kusema kuwa wote wako mahabusu na kusubiri uchunguzi ukamilike na kufikishwa mahakamani.
Alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 10 jioni  eneo la Chanika baada ya watu waliokuwa wakienda shambani kugundua mwili wa marehemu ukining’inia juu ya mti.
Akitoa wito kwa jamii kamanda huyo aliwataka watu kuacha kujichukulia sheria mikononi na kuacha kufanya vitendo viovu vya visasi na kusema kuwa polisi itawachukulia hatua kali za kisheria watu watakaofanya matukio kama hayo.
                                                        Mwisho

No comments:

Post a Comment