Kumekucha blog
Pemba, WAKAZI wa mji wa Wete Wilaya ya
Kaskazini Pemba, wamesema kero ya upatikanaji wa maji safi majumbani haitoisha
hadi Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) kukarabati miundombinu yake ambayo imezidi
kuwa chakavu.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi nyakati
tofauti, wakazi hao wamesema kero ya maji mjini humo imekuwa kero na kushindwa
kuwafikia majumbani baada ya njia nyingi za mabomba yanayopitisha maji kupasuka.
Wamesema hali hiyo imekuwa ikiwalazimu kwenda mabondeni
ambako pia upatikanaji wake umekuwa wa shida baada mabonde mengi kukauka maji
kutokana na kiangazi.
“Sisi huku kizimbani maji hayafiki kabisa na
tumeshazoea tukiamka tunakimbilia mabondeni---mabomba mengi yamepasuka na maji
yanaishia njiani na hili tumelisema sana” alisema Amran Hamis
“Tumetoa taarifa kwa mamlaka yetu ya maji kama inavyojulikana kwa jina la zawa----lakini chakushangaza wao pia
wanalitambua na kila siku wanatuambia watabadilisha mabomba” alisema
Akizungumzia kwa undani kero hiyo mkazi wa Chasasa, Said
Bakar, alisema wamekuwa katika wakati
mgumu kuweza kukabiliana na shida hiyo hasa vipindi vya watoto kwenda shule baada
kusongomana katika visima bondeni.
Alisema vipindi vya shule maeneo ya mabondeni watoto
wamekuwa wengi na kila mmoja kutaka kuwahi shule na hivyo kusubiria hadi saa 2
jambo ambalo nao wamekuwa wakichelewa kwenda katika majukumu yao kwa wakati.
Aliishauri Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) kuifanyia
ukarabati miundombinu yake ili kuweza kupata maji majumbani jambo ambalo maji
mengi yamekuwa yakipotea baada ya mabomba kuwa chakavu.
“Nashauri tu mamlaka yetu ikafanya ukarabati taratibu
angalau tuweze kupata maji kidogo kidogo vyenginevyo shida hii itatukondesha na
kutuchosha” alisema Bakar
Alisema kwa muda mrefu wamekuwa walilalamika na
kushindwa kilio chao kupatiwa ufumbuzi na hivyo kusema ni muda muafaka wa sasa
kuweza kupatiwa ufumbuzi kwani limekuwa la muda mrefu.
No comments:
Post a Comment