Eti Kanye West anawafunika mastar wengine wa kiume kwa mavazi?
Nilishawahi kusikia watu wakisema eti
jamaa hajui kupangilia mavazi, ana mtindo wa kuvaa ambao hauvutii na
ukimuangalia unaona kwamba ni kama hajali kuhusu mavazi yake.
Jarida la GQ wamefanya tafiti zao na watu wamepiga kura, majibu yemeonyesha kuwa rappa Kanye West, ndiye bingwa wa kutupia swaga kwa mwaka 2014.
Jamaa waliofanya tafiti wamesema mavazi
ya Kanye West yametafsiri na kubadili mazingira ya fashion kwa wanaume
wengi, mavazi yake ni kama yamekuwa yakielezea kesho zaidi kwenye Dunia
ya mitindo.
Kwenye utafiti huu, Kanye kawashinda mastaa wengi ikiwemo staa wa movie ya ‘Long Walk to Freedom‘ , Idris Elba.
Je unakubaliana na tathimini za Jarida la GQ kuwa Kanye West ndio ameleta mapinduzi katika mtindo wa uvaaji kwa wanaume 2014?
No comments:
Post a Comment