MWAKYEMBE ARIDHIA HATUA ZA SUMATRA KUIFUNGIA SAFARI MELI YA MV.VICTORIA KUTOKANA NA HITILAFU ILIYONAZO
Waziri wa uchukuzi Harrison Mwakyembe ameridhia hatua ya
mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini ( SUMATRA ) ya kuzuia
safari za meli ya Mv.Victoria katika ziwa victoria, baada ya meli hiyo
kugundulika na hitilafu mbalimbali zinazoweza kuhatarisha maisha ya
abiria.
Mwakyembe ameridhika na hatua hiyo baada ya uongozi wa bandari ya Mwanza kumtembeza sehemu mbalimbali za meli hiyo kongwe iliyotengenezwa
toka mwaka 1960, na kujionea jinsi mitambo yake ilivyochakaa kutokana
na kufanya safari zake kati ya miji ya Mwanza na Bukoba kupitia bandari
ya Kemondo ambapo amesema Serikali haiwezi tena kurudia makosa,
yaliyosababisha meli ya Mv.Bukoba kuzama na kupinduka mei 21 mwaka 1996
na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 800.
Awali kaimu meneja wa kampuni ya huduma za meli nchini ( MSC ), Fabian Mayenga amesema kwamba meli hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria
1200 na tani 200 mizigo, katika ukaguzi uliofanywa na SUMATRA imebainika
kuwa haiwezi kuendelea kufanya safari zake hadi hapo itakapofanyiwa
matengenezo makubwa yanayokisiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni
mojahuku akisema vifaa kwa ajili ya matengenezo hayo vitawasili nchini
katika muda wa wiki 12 hadi 15 ili meli hiyo ianze kuendelea kuhudumia
wananchi.
Akiwa katika uwanja wa ndege wa mwanza kukagua mradi mkubwa wa
upanuzi na ukarabati wa uwanja huo unaofanywa na kampuni ya Beijing
Construction Engineering group kwa gharama ya shilingi bilioni 105, Waziri huyo wa uchukuzi Harrison Mwakyembe amesema Serikali
inasikitishwa kulipa deni la shilingi bilioni 140 ambalo limesababishwa
na ufisadi wa baadhi ya watumishi wa shirika la ndege nchini ( ATC ),
huku akisema serikali inaendelea kukaribisha mashirika mengine ya ndege
ili kuweka kwenye sekta ya usafiri wa anga.
No comments:
Post a Comment