Friday, April 3, 2015

ARSENAL YAONGOZA KUNYAKUA TUZO

Oliver Giroud, Arsene Wenger kwenye tuzo hii ya ligi kuu England

giroudChelsea ndio vinara wa ligi kuu ya England kwa kuongoza huku ikiwa na pointi 67 mkononi lakini unaambiwa licha ya Arsenal kushikilia nafasi ya tatu imeweza kufanya vizuri na kuibuka na tuzo za kila mwezi kwa kufanya vizuri.
Mshambuliaji wa Arsenal Oliver Giroud amefanikiwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Machi katika ligi kuu ya England baada ya kazi yake nzuri akiwa na kikosi hicho.
Giroud raia wa Ufaransa amepata tuzo ikiwa ni ya 16 tangu kuanza kutolewa.
wengerNaye kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amefanikiwa kutwaa tuzo ya kocha bora wa ligi kuu ya England kwa mwezi Machi ikiwa ni mara ya 14 kwake kutwaa tuzo hiyo.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment