Friday, April 3, 2015

KIZUNGUZUNGU

Alex Ferguson kamtaja staa wake bora kwa soka, anamlinganisha na akina Ronaldo na Messi

Fergusson Thubs Up
Kumekuwepo na ushindani mkubwa kuanzia uwanjani mpaka mtaani, nani mkali kati ya Lionel Messi na Christiano Ronaldo.
Ronaldo anaaminika ndiye mchezaji bora duniani na hivi karibuni alibeba tuzo ya mwanasoka bora ya Ballon d’Or, lakini wapo wanaoamini Messi ndiye bora zaidi akiwemo mkongwe wa soka Pelle.
Kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson kaenda hatua moja mbele, yeye kasema kwamba Mbrazil Neymar Da Silva Santos ndiye mchezaji ambaye anaweza kusumbua vichwa vya mastaa hawa katika nafasi ya Mchezaji bora wa soka duniani.
.
Neymar Da Silva Santos
Ferguson alisema Neymar ni mchezaji anayebadilika kila siku na amekuwa akisumbua vichwa vya wengi, kwa upande wake anaona ndiye mchezaji anayeweza kushindanishwa na Ronaldo na Messi katika kwenye nafasi ya mwanasoka bora wa dunia.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment