Saturday, April 18, 2015

DAMU YAZIDI KUMWAGIKA KWA WAGENI AFRIKA KUSINI

Kingine kutoka Afrika Kusini.. Japo Rais kaingilia kati hali bado si shwari

150416123224_south_africa_xenophobia_640x360_afp
Bado hii ni ishu kubwa Afrika Kusini, vyombo vya habari vya Kimataifa kama BBC, Al Jazeera wameendelea kuiripoti kila wakati.. Inahusu ishu ya ubaguzi ambapo wageni yani wahamiaji wa kutoka nchi nyingine wanavamiwa, wapo waliouawa, wengine wamejeruhiwa.. ripoti zinasema wenyeji wanavamia maduka ya wageni hao na kufanya uhalifu.
Kingine kilichoripotiwa jana April 17 kinahusu mabalozi wa nchi mbalimbali za Afrika ambao wako South Africa walikutana Johannesburg kujadili kuhusu hali ilivyo nini kifanyike.
Ripoti zinaonesha machafuko hayo yamesababisha vifo vya watu sita.
Wahamiaji walifunga maduka yao kukwepa ghasia hizo, ingawa Polisi wameweka ulinzi lakini raia hao waliendelea kuwashambulia raia wa kigeni kwa lengo la kuwafukuza nchini humo.
Rais Jacob Zuma alihutubia nchi hiyo kupitia Bunge hotuba ambayo imekosolewa na wapinzani wake.
Hata hivyo Serikali ya Afrika Kusini imeahidi usalama kwa raia wa kigeni nchini humo huku kambi ya wakimbizi  iliyoko Kwazulu Natal ikizidi kufurika raia wa kigeni waliokimbia machafuko.
Hii ilikuwa moja ya taarifa zilizoripotiwa na kituo cha K24 Kenya,

No comments:

Post a Comment