Yuko selo anasubiri hukumu ya kesi yake, kesi nyingine kajiongezea humohumo..
Ukishakuwa
chini ya ulinzi kituo cha Polisi kuna vitu ambavyo hauko huru kufanya
kwa sababu tu ya sheria za maeneo hayo.. hii stori iko kwenye headlines
za vyombo vya habari kule Kenya, mitandao imeandika pia.
Inamhusu Henry Magee, alikuwa anashikiliwa na Polisi kwa kesi ya kumteka mwanafunzi wa kike.
Kesi ambayo iliongezeka kwa huyu bwana
ilikuwa ni ishu ya kuvuta sigara akiwa selo.. akafikishwa tena
Mahakamani na kutozwa faini ya Sh 15,000 za Kenya katika Mahakama ya
Eldoret baada ya kukubali kufanya kosa hilo.
Mtuhumiwa huyo Henry Magee alitozwa faini hiyo na Hakimu Tom Olando,
ambae amesema alisikia harufu ya moshi wa sigara akiwa kwenye chumba
chake cha kusikilizia kesi, chumba hicho kiko jirani na selo ambayo Henry alikuwa amefungiwa.
Jamaa alipewa nafasi ya kujitetea; “Ni kweli nilifanya makosa ambayo yametajwa dhidi yangu lakini ni kwa sababu ya mazoea ya kutumia sigara,”– Magee.
Kitu ambacho nimejiuliza ni kwamba watu
wengi akishakua yuko selo anakuwa na uoga hivi, sasa huyu jamaa kapataje
ujasiri wa kuvuta sigara kabisa ndani ya chumba cha jela !!
Hutopitwa na habarii yoyote inayonifikia na niko tayari kukutumia muda wowote kupitia hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment