Ni kweli ulaji wa kuku wa kisasa unafifisha nguvu za kiume? ninae Daktari mwenye majibu yake hapa
Siku
zinazidi kusogea, maisha yanazidi kupata ugeni mkubwa wa vitu
mbalimbali ambavyo vinakuja kutajwa kitaalamu kwamba ni hatari kwa mwili
wa binadamu.
Daktari aliyetangazwa kushika namba moja Tanzania kwenye maswala ya kijamii Dr. Isack Maro anaesikika leo katika moja ya vituo vya radio na kueleza kuwa kuna ukweli gani kuhusu ishu
iliyotajwa kwamba kuku wa kisasa ana madhara kwenye mwili wa Mwanaume na
anafifisha nguvu za kiume.
Dr. Isaac
anaanza kwa kusema >>> ‘Hii ni changamoto ambayo haipo
Tanzania peke yake, ulimwenguni ni moja ya changamoto na mjadala mkubwa
unaendelea, kuna wale wanatetea haki za walaji na wale ambao wanafanya
biashara’
‘Kuku analiwa kuliko mnyama au ndege yeyote duniani, wanasema kwa mwaka kuna kuku milioni 55 ambao wanaliwa zaidi ya ukikusanya pamoja, Mbuzi, Ngo’mbe na Nguruwe’
1. >>>
‘Mbinu ndio zinazoleta madhara, ni mbinu za kisayansi kuhakikisha
kwamba kuku anakua na uzito wa kutosha katika kipindi cha wiki tatu,
aweze kunona na kuuzika kirahisi’
2. >>>
‘Ukweli ni kwamba kinacholeta madhara sio nyama ya kuku bali ni vile
vitu ambavyo vimewekwa kwenye kuku kuhakikisha kwamba kuku huyu anakua,
anaongezeka uzito na mengine…….. na bahati mbaya huwa hizi ni kemikali
au dawa mbalimbali’
3. >>> ‘Hizi
dawa nyingine sio nzuri kwa mwili wa Mwanadamu hata kwa mwili wa kuku
mwenyewe ni vile tu kuku hatumuoni sababu ameshachinjwa’
4. >>>
‘Ili Mwanaume aweze kuwa na nguvu za kiume anahitaji kuwa na uwiano wa
kutosha na mzuri katika mfumo wake wa fahamu, wa damu na mwili wake
mzima’
5. >>>
‘Moja kati ya vitu vinavyohitajika kwa wingi kwa Mwanaume ni homoni ya
kiume ambapo bahati mbaya sana moja ya kemikali zinazopatikana kwa kuku
ni homoni zinazomsaidia akue, hizi zikiingia kwenye mwili wa Mwanadamu
zinavuruga utaratibu mzima wa mwili kutengeneza homoni, kuna uwezekano
mkubwa kabisa ile homoni ya kiume isitengenezwe kwa wingi, hapo ndio
tatizo linakoanzia’
6. >>>
‘Tulizungumzia zamani Wanaume kuwa wanaota vitu kama Matiti, wananenepa
kwenye sehemu ambazo hazitakiwi kunenepa kwa sababu ile homoni ya kiume
imevurugwa, lakini pia kwa sababu homoni/kemikali tunazomuwekea Kuku ni
nyingi kunatokea mvurugano mkubwa kabisa unaovuruga mfumo wa fahamu wa
mwili’
Hutopitwa na habari yoyote inayonifia na niko tayari kukusogezea kila kinachonifikia hapa hapa www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment