Ndege ya kipekee inayotumia nguvu ya jua ilikwamia China, kitu kimoja tu kimeikwamisha (picha 10).
Ni
ndege ambayo ilianza safari yake March 9 2015 Abu Dhabi na ikafanikisha
salama safari zake kwa kupaa angani na kupita Oman, India na Myanmar.
Marubani wawili wanaoiendesha wanasema
wanataka kuvunja rekodi kwa kuuthibitishia ulimwengu kwamba Ndege
inayotumia nguvu ya Jua inaweza kutumika kwenye dunia ya sasa.
Pamoja
na hayo, safari yao bado ni ndefu ambapo siku mbili zilizopita
waliripotiwa na CNN kwamba safari yao imekwama China kwa zaidi ya wiki
mbili baada ya kushindwa kupaa kutokana na hali mbaya ya hewa, hali
ikiwa mbaya inavunja masharti ya kuipaisha ndege hii.
Jamaa
wamepanga kuzunguka na hii ndege kwenye nchi mbalimbali za dunia lakini
bila kutumia hata tone moja la mafuta, yani wanataka itumike nguvu ya
jua kama ndege ilivyoundiwa.
Yote haya utayapa hapa hapa tangakumekuchablog usiwe mbani nami
No comments:
Post a Comment