Sijawahi kusikia marubani wamepigana ndani ya ndege, hii imetokea India
Bado
hatujausahau msiba wa ndege ya Ujerumani kuangushwa na Rubani msaidizi
kwa makusudi Ufaransa na kuua zaidi ya watu 150 ndani yake, sasa tunayo
hii nyingine kutoka India.
Shirika la ndege ya Air India
limewasimamisha kazi marubani wake wawili baada ya kudaiwa kupigana
ndani ya chumba cha Marubani kwenye ndege hiyo iliyokua na safari ya
kutokea Delhi kwenda Jaipur.
Japo
shirika lenyewe linasema kilichotokea ni kurushiana matusi, habari za
uhakika kwenye vyanzo vingine zimeonyesha jamaa hawa walipigana na
Rubani Msaidizi ndio anadaiwa kuwa chanzo cha kulianzisha, yani Captain
(Rubani mkuu) alimuagiza kurekodi data ikiwemo kufahamu ni abiria
wangapi wapo ndani ya ndege kabla hawajapaa hapo ndio ugomvi ukaanzia.
Hii ishu imetokea wakati headlines za ndege
2015 zikiwa kwenye wiki yake nyingine tena toka ndege ya Ujerumani
iangushwe kwa makusudi na Rubani Msaidizi March 24 2015 ambaye
alimfungia nje ya chumba cha Marubani, Rubani mkuu aliyekua ametoka nje
kwa wakati huo.
No comments:
Post a Comment