Shoka likatumika kuyakatili maisha ya mtoto.. Ilikuwa Birthday ya baba yake mzazi
Tunaona ndoa nyingi zinavunjika, kila
mtu anaenda upande wake alafu maisha yanandelea.. Mara nyingi waathirika
wa matukio ya aina hii ni watoto, hii ishu imetajwa mara nyingi pia
kwamba inasababisha sana kuwepo kwa ongezeko la watoto wa mitaani kila
siku.
Hii ni ya kusikitisha kidogo, mwanamke mmoja Mexico ambaye jina lake ni Karina Luna Sandoval hakuwa
na raha kwa kitendo cha kutelekezwa na mzazi mwenzake ambaye walizaa
nae mtoto mmoja ambaye alikuwa tayari ana umri wa miaka 7.
Akampata mpenzi mwingine, Gonzalo del Rio Hernandez wakashauriana
eti waandae zawadi ambayo watampa jamaa ambaye alimzalisha mwanamke
huyo na kumtelekeza.. walivyoshauriana wakaona zawadi ambayo jamaa
hatoisahau ni kumuua mtoto huyo.
Akampeleka mtoto huyo kwenye bustani akamwambia amsubiri baba yake anakuja, hiyo ilikuwa December 20 2015, akatokea Gonzalo na shoka dogo akaanza kumpiga mtoto huyo kwa lengo la kumuua.
Watu walisikia kelele za mtoto huyo
akiwa analia, wakafanikiwa kuwakamata mwanamke huyo pamoja na mpenzi
wake huyo ‘mpya’, Ambulance ikamchukua mtoto kumpeleka Hospitali, lakini
kwa bahati mbaya wiki mbili baadae akafariki.
Karina na Gonzalo walikiri kufanya kosa hilo, hukumu iliyotolewa na Mahakama ni kifungo cha miaka 42 jela kwa Karina na mpenzi wake huyo amefungwa kifungo cha miaka 40.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment