Huenda na wewe hukutarajia hii ingetokea kwa mtu aliyekamatwa kituo cha Polisi
Labda
isingekushtua kusikia tukio la mtuhumiwa kuuawa baada ya kukamatwa na
watu wenye hasira, lakini hii ya mtuhumiwa kukutwa amefariki akiwa
mikononi mwa Polisi iko tofauti kidogo.
Mara nyingi tunaona watuhumiwa
wakikamatwa, baada ya kufikishwa kituo cha Polisi wanasachiwa na kuacha
kila kitu kwenye meza ya Askari ili kama ana kitu kibaya asijidhuru
akiwa amefungiwa jela, uliwahi kudhani kwamba kuna mtuhumiwa atakuja
kujiua kwa nguo zake alizoingia amezivaa?
Imetokea Masvingo Central Police,
kituo cha Polisi kilichopo Zimbabwe ambapo mtuhumiwa mmoja amejinyonga
akiwa ndani ya jela ya kituo hicho cha Polisi kwa kutumia T-shirt
aliyokuwa amevaa, mtuhumiwa huyo alikuwa amekamatwa kwa makosa ya
kumbaka mtoto wa kaka yake, kumpa ujauzito na kumuambukiza HIV.
Jamaa huyo Nevison Tapesana alikutwa akiwa amejinyonga siku moja tu baada ya kufikishwa na kuhojiwa kuhusu mashtaka hayo kwenye Kituo hicho.
Police walishtuka kumkuta asubuhi akiwa
ananing’inia dirishani huku akiwa amejinyonga kwa T-shirt ambayo
aliingia nayo akiwa ameivaa.
Tapesana anahisiwa pia kuhusika na tukio la kubakwa na kuuawa mwalimu mmoja wa Chuo, hiyo ilitokea kama mwezi mmoja uliopita.
No comments:
Post a Comment