Sunday, April 5, 2015

SOMA MAKUBWA YALIANDIKWA MAGAZETINI LEO, APRIL 05

Uchambuzi huu wa magazetini unaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya Kituo Cha Elimu Cha Candle Education Tanga. Kituo kinaongoza kwa kufaulisha wanafunzi wanaorisiti. Kituo kimesajiliwa na NECTA. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746

this-weekendNIPASHE
Sakata la msichana wa Kitanzania, Ummul- Khayr Sadri Abdulla ambaye amedaiwa kutaka kujiunga na kikundi cha ugaidi cha Al-Shabaab linazidi kuchukua sura mpya baada ya madai kuwa alitoroka  chuoni Sudan wiki moja kabla ya kukamatwa Kenya.
Msichana huyo mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa Afrika kilichopo Sudan alikuwa akisomea udaktari mwaka wa tatu, kabla ya kukamatwa Machi 30 mwaka huu alikuwa ameshatoroka chuoni  hapo tangu Machi 22 na ndugu zake walikuwa wanamtafuta.
Akizungumza na gazeti la NIPASHE babu wa msichana huyo Nassor Said Nofli, alisema kuwa taarifa za kupotea zilitolewa na dada yake mkubwa ambaye pia anasomea udaktari mwaka wa nne katika chuo hicho kitu ambacho kiliishtua familia hiyo.
Babu huyo amesema ilipofika Jumanne ilitolewa taarifa kwa baba yake aliyeko Oman kikazi, Dk. Sadri Abdulla Said pamoja na ndugu wengine waliopo Pemba, Unguja na Dar es Salaam.
Hizi taarifa za kupotea kwa binti yetu zilitushtua na ilitulazimu kuomba maombi maalum ya kumuombea “Dua” ili aweze kuonekana na akiwa salama kwa sababu Sudan kama unavyoielewa ni nchi yenye matatizo ya kivita ” alisema babu huyo.
Kitendo cha polisi kumkamata imetusaidia na pia wamesaidia kumuokoa yule mtoto kutokujiingiza kwenye hicho kikundi kwani angeweza kuuliwa ama kupotea katika kundi hilo,”– Nofli.
Alieleza kuwa mbali na binti wao kuendelea kushikiliwa na polisi, wanaamini kuwa vyombo vya sheria vitatenda haki.
Kadhalika alisema jambo lingine lililoishtua familia yake ni pale vyombo vya habari vilivyoeleza kuwa wazazi wa binti huyo ni wahadhiri wa chuo hicho ambacho watoto hao wanasoma jambo ambalo si la kweli.
Taarifa kutoka kwa Kamishna wa Polisi Jimbo la El –Wak Kenya, Nelson Marwa zinaonesha kuwa wasichana hao watatu walikuwa wanakwenda Somalia kupata mafunzo ya kigaidi na baadaye kufanya mashambulizi ya kujitoa mhanga.
Kutokana na kuwepo taarifa kwamba msichana huyo alikuwa anakwenda kuolewa na Askari wa Kikundi hicho cha kigaidi, Mkurugenzi wa Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Hellen Kijo Bisimba alisema kama alikwenda kuolewa haina haja ya kukamatwa kwani suala la ndoa lipo kijamii.
Hata hivyo, mpaka sasa wasichana hao bado hawajafunguliwa mashtaka yoyote japo mahakama ya nchini humo imeliruhusu jeshi la polisi kuwashikilia kwa siku 20 kwa ajili ya upelelezi.
HABARI LEO
Siku chache baada ya kuzinduliwa kwa treni mpya ya Deluxe abiria wa kwanza kusafiri kwa treni hiyo kutoka Dar kwenda Kigoma wamefanya uharibifu katika baadhi ya mabehewa ikiwemo kung’olewa kwa mikono ya kuoandishia na kushusha vitanda pamoja na kong’olewa kwa mapazia.
Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Reli TRL, Midraji Maez amesema Shirika hilo litawachukulia hatua za kisheria watakaobainika kuhusika na uharibifu huo.
Uharibifi huo umefanywa kwenye mabehewa mazuri ya treni hiyo mpya ambayo ina huduma ya Internet, swichi za umeme kwa ajili ya kuchajia simu, pamoja na siti ambazo kila abiria anakaa kwenye siti yake.
Mmoja wa wananchi wa Kigoma amelaani kitendo ha uharibifu uliofanyika kwenye treni hiyo.
NIPASHE
Askofu Gwajima anatakiwa kuripoti muda wowote kuanzia leo katika Hospitali ya TMJ kwa uchunguzi zaidi baada ya kuisha kwa muda ambao alipewa kwa ajili ya kupumzika.
Tulimpa muda wa wiki moja, hadi sasa muda umekwisha, hivyo wakati wowote anatakiwa kuripoti Hospitalini ili kuangaliwa maendeleo ya hali yake na kama haijaimarika, tutamchunguza zaidi”—Dk. Fortunatus Mazigo, daktari ambaye anamtibu Askofu huyo.
Daktari huyo amesema hawezi kuuzungumzia ugonjwa ambao anaumwa Askofu huyo kutokana na maadili ya kazi yake, ila akipata ruhusa kutoka kwa mhusika mwenyewe atafanya hivyo.
MTANZANIA
Ndoa ya Dk. Mengi ana Jacquiline Ntuyabaliwe ambayo ilifungwa kwa siri Mauritius ana kuhudhuriwa na marafiki wachache takribani 50 imezua gumzo.
Safari ya wawili hao kuelekea uchumba ilianza Desemba mwaka 2014 ambapo walivalishana pete za uchumba katika sherehe za kumbukumbu ya kuazaliwa ya Jacquiline iliyofanyika Dubai.
Rafiki wa karibu na Jacquiline, Nancy Sumari aliweka picha katika ukurasa wake wa Instagram ikimuonesha Jacquiline akirusha juu maua pamoja na rafiki zake akiwemo Faraja Kota, Nasreen Kareem na Sophia Byanaku.
Mengi na Jacquiline tayari wana watoto mapacha ambao nao pia walihudhuria ndoa ya wazazi wao.
MWANANCHI
Hofu imewakumba waumini wa Kanisa Katoliki Kisarawe baada ya muumini mmoja kukutwa akiwa na bastola na risasi nane katikati ya ibada.
Polisi pamoja na waumini walitoa taarifa kwamba mwanaume huyo hakuwa muumini wa kanisa hilo na alikuwa akipanga kufanya uhalifu.
Waumini wa kanisa hilo wamesema jamaa huyo aliingia mapema kabla ya ibada kuanza, baadaye akawa anahamahama na mara nyingine alikuwa akitoka nje kufanya mawasiliano.
Ni mara ya kwanza kutokea kwa tukio kama hili na hatujajua alikuwa na lengo gani”—alisema Padri wa Kanisa hilo, Padri Kirimo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Urich Matei amesema mtuhumiwa huyo alikutwa na bastola pamoja na risasi nane, Jeshi la Polisi linamshikilia kwa mahojiano zaidi.
Kamanda Matei amesema mtuhumiwa maelezo ya awali amesema kwamba yeye ni mkazi wa Mburahati na wakati mwingine amesema ni mkazi wa Mkuranga na kazi yake ni mkandarasi.

No comments:

Post a Comment