Uchambuzi huu kutoka magazetini unaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga. Kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita. Pia kinatoa kozi za Kiingereza na Computer. Chuo kimesajiliwa na NECTA. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 7727246
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe
amesema Ubalozi wa Tanzania uliopo Kenya unafuatilia kama kama kuna
wanafunzi wa Tanzania waliojeruhiwa ama kuuawa katika shambulio la
kigaidi lililoua zaidi ya wanafunzi 147 Chuo Kikuu Garissa.
“Kuhusu
suala hilo nitatoa taarifa hiyo kesho (leo) baada ya kupata taarifa
rasmi wa nchini humo.. nitatoa kwa kuita waandishi wa Habari au kutuma
taarifa tu..”—Waziri Bernard Membe.
Waziri huyo amesema kuwa mpaka sasa
hajapata taarifa yoyote kuhusiana na hilo japo Ubalozi wa uliopo nchini
humo unaendelea na jtihada kujua kama kuna Watanzania wameathirika.
HABARI LEO
Mamlaka ya SUMATRA imesema itatoa majina
na picha za madereva wanane waliowafutia leseni kutokana na kusababisha
ajali kwa uzembe na hawataruhusiwa kuendesha mabasi ya abiria.
“Madereva
hao ni wale waliosababisha ajali za vifo mwezi uliopita na kuanzia sasa
kila mwisho wa mwezi tutatoa idadi ya madereva watakaokuwa wamefutiwa
leseni kutokana na makosa hayo ili kuweza kudhibiti ajali nchini”—David Mziray, Meneja Mawasiliano wa SUMATRA.
Mziray
ametoa pongezi kwa Jeshi la Polisi kudhibiti mwendo wa magari wa
kilometa 80 kwa saa katika jitihada za kupunguza ajali ambapo amesema
kwa sasa basi za kutoka Mwanza zinalazimika kutembea kwa siku mbili
kufika Dar.
MWANANCHI
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT, Zitto Kabwe
ameweka hadharani utajiri wake akisema ana fedha taslimu Mil.18 na
nyumba mbili zenye thamani y ash. Mil. 223 zilizopo Mwandiga, Kigoma
ambapo alitangaza hivyo kutimiza matakwa ya Katiba ya Chama hicho.
Mbali na hivyo Zitto
pia ana gari aina ya ya Freelander yenye thamani ya Mil. 74, huku
akisema ametimiza masharti hayo ikiwa ni siku ya tano baada ya kuia
saini hati ya makubalian ya Chama hicho.
“Huwa
napata kipato cha kutoka ndani na nje ya Tanzania. Nina mkataba wa miezi
zita na Shirika la Twaweza kwa malipo ya dola ya Tshs. Mil. 3.7 kwa
mwezi”— Zitto Kabwe.
Kutokana na fomu aliyojaza Zitto
imeonesha pia ana madeni ya jumla ya Mil. 174.6 ambako alichukua mikopo
ambayo ni stahiki kwa Mbunge.
MWANANCHI
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Kibondo Kigoma amemhukumu Diwani wa Kata ya Kasanda Wilaya ya Kakonko, Dickson Barutwa
na wenzake watatu kufua mashuka ya katika Hospitali ya Wilaya na
kusafisha mitaro kwa siku 14 baada ya kukutwa na hatia kwenye makosa
matatu.
Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Peter Makala
alisema mashtaka yaliyokuwa yanawakabili watuhumiwa hao ni kosa la
kuingia eneo la Ofisi ya Mtedaji wa Kijiji na baadaye kufunga kufuli
mlangoni na kuweka gundi na unga wa ngano kumzuia Mtendaji kufanya kazi.
Watuhumiwa hao waliamriwa kulipa faini
Sh. 50,000/= kila mmoja au kufungwa jela miezi mitano kila mmoja,
watuhumiwa wote walikubali kulipa faini isipokuwa Kasase ambaye
anakabiliwa na kesi nyingine ya mauaji.
Hakimu huyo amesema washtakiwa wana
adhabu ya kufanya kazi za kijamii ambapo walikabiidhiwa kwenye Idara ya
Maendeleo ya Jamii Wilaya hiyo.
Kaa karibu nami tangakumekucha.blogspot.com, nitakachokipata nitakusogezea hapa hapa.
No comments:
Post a Comment