Uvamizi wa kigaidi kwenye Headlines Kenya.. Hii imetokea Chuo Kikuu leo
Kumekuwa
na Headlines za story nyingi kutoka Kenya zinazohusu mashambulizi ya
kigaidi katika maeneo mbalimbali ambapo matukio hayo yanahusisha sana
kikundi cha Kigaidi ccha Al-Shabaab, leo kuna tukio jingine kwenye Headlines kuhusu mashambulizi ya aina hiyo.
Ripoti iliyotoka mpaka sasa inasema watu wawili wameuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa kutokana na tukio la uvamizi Garissa College University, walioshuhudia wanasema watu waliovamia haijafahamika idadi kamili ila ni kati ya watu sita na kumi.
Wavamizi hao walikuwa na silaha ambapo
imesikika milio ya risasi kutoka kwenye Chuo hicho kilichopo karibia na
mpaka wa Kenya na Somalia.
No comments:
Post a Comment