Wazazi waliingilia ndoa ya mtoto wao, mkwe akaona alipize kisasi kwenye chai
Migogoro
kwenye ndoa wengine wanaona ni kawaida, wengine huwa inawachosha.. Ziko
story utasikia wanandoa wamepigana, wengine wanaachana.
Nimeipata hii stori toka India, Rekha Nagvanshi ni mwanamke ambaye ameonekana kuchoshwa na manyanyaso ya mume wake, kuna wakati waliachana.. baadae wakarudiana.
Baada ya kurudiana makubaliano ilikuwa
hivi, mume awe anahusika na majukumu yote ya nyumbani yani kuanzia kufua
nguo, kuosha vyombo.. kupika.
Wazazi waliingilia kati na kufanya makubaliano hayo yakavunjika, Rekha hakuridhika wazazi kuingilia kati masuala yao ya ndoa.
Rekha alikutwa na mama mkwe wake
akikojolea kwenye birika la chai jikoni, rafiki yake anasema labda kwa
vile alikasirishwa na wazazi hao ndio maana akaamua alipize kisasi kwa
kufanya hivyo.
Wazazi hao wamesema walikuwa wanajua
mkwe wao hawapendi lakini hawakufikiria kama angeweza kuwafanyia kitendo
hicho, walienda kutoa taarifa Polisi lakini majibu ya Polisi
waliwaambia hawashughulikii kesi za namna hiyo.
Mume wa mwanamke huyo ambaye anaitwa Deepak amesema yeye aliridhika na masharti ya mke wake waliporudiana lakini wazazi wake hawakupenda kuona anafanywa kama mtumwa.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment