Fahamu timu za Mastar kwenye ligi ya England.
Soka ni mchezo unaopendwa duniani kote na imezoeleka kwamba ni mchezo ambao mara nyingi hufuatiliwa na watu daraja la kati na daraja la chini huku watu wa daraja la juu ambao wengi ni matajiri na watu maarufu wakiwa hawana muda wa kufuatilia mchezo huu .
Hata hivyo ukubwa wa soka unaweza kuwa umetazamwa kwa jicho la kawaida kwa uhalisia ni kwamba nguvu ya mchezo huu ni kubwa kiasi kwamba hata watu maarufu wameshindwa kuepuka wingu la ushabiki wake.
Katika hali ya kawaida ligi ya England ndio ligi inayopendwa na kufuatiliwa na idadi kubwa ya watu duniani na timu zake kubwa kama Manchester United , Arsenal , Liverpool na Chelsea zikiwa na idadi kubwa ya mashabiki nje ya England kuliko hata klabu za Barcelona na Real Madrid .
Cha kushangaza ni kwamba kuna idadi kubwa ya watu mashuhuri ambao wanaufuata mchezo wa soka kuliko ambavyo mtu anaweza kudhani na watu hawa wanashabikia timu ambazo huwezi kuamini .
Waziri mkuu wa Enland David Cameroon pamoja na kutingwa na shughuli za siasa ni shabiki wa kutupwa Aston Villa .
Cameroon anaungwa mkono katika ushabiki wake wa klabu hii na Mjukuu wa Malkia Elizabeth Prince Harry ambaye ni shabiki wa Aston Villa pia .
Baba yake Prince Harry ambaye ni Prince Charles ni shabiki wa Burnley klabu ambayo rangi za jezi yake inafanana na rangi za jezi ya Aston Villa .
Nyota wa muziki wa Pop Justin Bieber amethibitisha kuwa shabiki wa klabu ya Everton na amepigwa picha akiwa na jezi za klabu hiyo huku akicheza mpira na wenzie .
Nyota wa muziki wa Hip-Hop Jay-Z naye hayuko nyuma kwenye masuala ya soka na amekiri kuwa shabiki mkubwa wa klabu ya jijini London ya Arsenal .
No comments:
Post a Comment