MBIO
ZA SAKAFUNI HUISHIA UKINGONI 24
ILIPOISHIA
Waziri
Mkuu akamueleza kwamba kuna muuguzi ameuawa na daktari wake.
“Sawa
mheshimiwa, tunakuja”
Waziri
Mkuu alipomaliza kuzungumza na mkurugenzi wa upelelezi alitoka nje ya hospitali
hiyo akiwa amefuatana na mke wake.
Walikuta
Dk Deo amepakiwa katika gari la polisi huku mmoja wa polisi hao akiwasiliana
kwa radio Call na polisi wenzake.
Wasiwasi
wa Waziri Mkuu na mke wake ulikuwa kwa Sofia,
hawakujua lipotoka katika ofisi ya Dk Deo alikwenda wapi.
Lakini
walipokwenda kwenye gari lao walimkuta amejipakia katika siti ya nyuma na
alikuwa amelala. Kwenye mdomo wake wa chini alikuwa na chembechembe za damu.
SASA
ENDELEA
Mke
wa Waziri Mkuu alifungua mlango wa gari akajipakia. Alifungua mkoba wake akatoa
kitambaa na kuifuta midomo ya Sofia
kisha alikikunja kitambaa hicho na kukirudisha kwenye mkoba.
Waziri
Mkuu hakuingia kwenye gari. Alibaki nje ya gari akihaha huku na huku. Baadhi ya
wauguzi na madaktari walikuwa wakitoka na kuingia ndani ya hospitali hali
iliyoonesha taharuki.
Hakukuwa
na yeyote miongoni mwao aliyefahamu nini kimetokea.
Muda usio
mrefu, magari matatu ya polisi na makachero yakawasili. Gari la kwanza lilikuwa
la mkurugenzi wa Upelelezi. Gari la pili lilikuwa na mchanganyiko wa makachero
na polisi na gari la tatu lilitoka kituo kikuu cha polisi baada ya polisi
walokuwa wakifuatana na Waziri Mkuu kuwapigia radio call.
Polisi
na makachero hao waliokuwa zaidi ya kumi walishuka na kusogea alipokuwa amesimama
Waziri Mkuu.
Waziri
Mkuu alimueleza Mkurugenzi wa upelelezi kuhusu tukio lililokuwa limetokea
akimuhusisha Dk Deo kumshambulia muuguzi wake.
“Polisi
wamemkamata, yuko kwenye hili gari” alimwambia huku akimuonesha gari hilo.
Akaongeza.
“Muuguzi aliyemfanyia unyama huo yuko ofisini kwake”
Mkurugenzi
wa Upelelezi alisogea kwenye gari hilo
akamtazama Dk Deo kisha alimwambia atoke kwenye
gari. Alipotopka alimwambia.
“Twende
ukatuoneshe
huyo muuguzi wako”
“Lakini
mimi sijamfanyia kitendo chochote kibaya, nilimkuta ofisini kwangfu akiwa ameshajeruhiwa” Dk Deo
alijitetea.
“Muongo
mkubwa. Nilimuona kwa macho yangu akimpopotoa” Waziri Mkuu alisema.
Mkurugenzi
wa Upelelezi akampiga kibao Dk Deo kabla ya kumwambia.
“Twende
ukatuoneshe
huyo muuguzi wako”
Kabla
ya Dk Deo kuinua hatua alitandikwa kibao kingine na kusukumwa. Mkurugenzi wa
Upelelezi alikuwa amemshika kiunoni.
Wakati
Dk Deo akiwapeleka ofisini kwake, Waziri Mkuu alifuata nyuma.
Walipofika
ofisini humo, Waziri Mkuu aliwaonesha yule muuguzi aliyekuwa amelala chini. Ile
damu iliyokuwa ikimvuja shingoni sasa ilikuwa imeganda.
“Huyo
achukuliwe apelekwe hospitali ya Muhimbili kufanyiwa
uchunguzi”
akawambia.
Baada
ya polisi kumkagua na kumpiga picha, walimbeba na kutoka naye. Alipakiwa kwenye
gari mojawapo la polisi. Dk Deo alipakiwa kwenye gari jingine.
Makachero
kadhaa pamoja na polisi walibaki pale hospitali na kuanza kuwahoji madaktari
wengine na wauguzi kuhusu kilichokuwa kimempata mwenzao.
Mwili
wa muuguzi huyo ulipelekwa hospitali ya Muhimbili. Dk Deo alipelekwa kituo
kikuu cha polisi. Waziri Mkuu, mke wake pamoja na Sofia waliondoka na kurudi nyumbani.
Walimuacha
Sofia aende akalale chumbani mwake. Waziri Mkuu na mke wake wakakaa sebuleni.
“Kama
nisingetumia mbinu ile ya kumsingizia yule
dakatari, leo Sofia
angebainika kuwa ndiye mfyonza damu na angekamatwa kutokana na ushahidi wa yule
dokta” Waziri Mkuu alimwambia mke wake.
“Angekamatwa
kwa sababu ingeonekana wazi kuwa ndiye aliyemfyonza damu. Aliondoka naye kule
chumbani akangoja alipoingia mle ofisini akamshika…”
“Hili
sasa limekuwa balaa!”
Mke
wa Waziri Mkuu akatikisa kichwa.
“Sijui
kama mwanangu atarejea katika hali yake ya kawaida!” alisema na kuongeza.
“Juhudi
kubwa zimefanyika lakini bado hali inatia mashaka, sijui tufanye nini?’
“Sijui
mke wangu, nimechanganyikiwa! Yaani nimelazimika kuokoa jahazi kwa kumbambikia
yule daktari kosa la Sofia”
“Kwani
atashitakiwa?’
“Lazima
ashitakiwe kwa mauaji, najua tutapambana sana mahakamani lakini
nitatumia kila mbinu kuhakikisha haepuki ile tuhuma”
“Sasa
Sofia tutampeleka wapi?”
“Tutamrudisha
kijijini akae huko huko chini ya uangalizi. Tutakodi watu wa kuwa naye wakati
wote kuhakikisha hafyonzi watu. Ile damu inaweza kumuua. Damu nyingine si
salama”
Ili kumkandamiza zaidi Dk Deo, Waziri Mkuu
alimpigia simu Waziri wa Mambo ya Ndani akamueleza kuhusu lile tukio akidai
alimshuhudia kwa macho yake Dk Deo akimfyonza damu muuguzi wake hadi kumuua.
Baada
ya kumpigia Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri
Mkuu alimpigia Mkuu wa Jeshi la Polisi.
“Nimeshapata taarifa mheshimiwa na hivi sasa tunalifanyia
uchunguzi tukio hilo” Mkuu wa Jeshi la Polisi alimwambia
Waziri Mkuu mara tu alipomdokeza kuhusu tukio hilo.
“Kama mmeanza kufanya uchunguzi ni vizuri. Yule mtu ni
katili sana”
“Kumekuwa
na matukio ya ufyonzwaji damu hapa nchini, tutachunguza kuona kama
ni yeye aliyehusika”
“Itakuwa
ni yeye, wasomi wengine wanafanya kazi zao kwa kutegemea ushirikina”
“Hilo suala tunalifanyia
kazi mheshimiwa”
“Tunataka
haki itendeke na mhakikishe kwamba anapelekwa mahakamani mara tu uchunguzi wenu
ukikamilika”
“Asante
mheshimiwa”
Wakati
huo hospitali ya Dk Deo ilikuwa imezingirwa na makachero na kuwekwa chini ya
ulinzi wa polisi. Mwili wa muuguzi aliyefyonzwa damu na Sofia ulifanyiwa uchunguzi haraka haraka
katika hospitali ya Muhimbili na matokeo ya uchunguzi huo yalitolewa kwa
polisi.
Uchunguzi
huo mbali ya kuthibitisha kifo cha muuguzi huyo ulieleza kuwa kifo hicho
kilitokana na marehemu kufyonzwa damu nyingi mwilini mwake kupitia katika
jereha lililokuwa kwenye shingo yake ambalo lilitokana na kuumwa meno ya
binaadamu.
Taarifa
hiyo ya madaktari ndio iliowapa polisi taharuki. Ile dhana kwamba Dk Deo ndiye
mfyonza damu za binaadamu iliwafanya polisi wamng’ng’anie kama
ruba.
Mbali
ya hospitali yake kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi, makachero walianza
kuwahoji madaktari na wauguzi wa hospitali hiyo.
Madaktari
na wauguzi wote waliohojiwa walieleza kuwa hawakuliona tukio hilo linalodaiwa kufanywa na Dk Deo.
Pia
walieleza kwamba hawaamini kuwa Dk Deo anafyonza watu damu.
Baada
ya kutoridhishwa na maelezo ya madaktari na wauguzi hao, makachero walianza
kuwahoji wagonjwa waliokuwa wamelazwa katika hospitali hiyo.
Wagonjwa
hao pia hawakuwa na maelezo ya kuwatosheleza polisi kuhusiana na tuhuma
zilizokuwa zinamkabili Dk Deo. Mkurugenzi wa Upelelezi akaja na dhana nyingine.
Aliwataka makachero hao kuifanyia upekuzi hospitali hiyo kwa hofu
kwamba Dk Deo anaweza kuwa ananunua viungo vya binaadamu ambavyo anavitumia
katika shughuli zake za kishirikina.
Upekuzi
huo ulifanywa lakini hakukuwa na kiungo chochote kilichopatikana.
Dk
Deo mwenyewe alihojiwa kwa saa kadhaa. Alichokuwa akikieleza kilikuwa
hakikubaliwi na polisi ambao tayari walishajenga hisia kwamba Dk Deo ni mfyonza
damu.
Dk
Deo alieleza kwamba wakati tukio hilo
linatokea hakuwepo ofisini. Lakini wakati anarudi ofisini mwake alimuona Sofia binti wa Waziri Mkuu
akitoka ofisini mwake.
“Nilipoingia
ofisini mwangu nikamuona muuguzi wangu akiwa chini huku akitokwa na damu
shingoni. Nilipomchunguza vizuri nikagundua kuwa alikuwa na jeraha ambalo
sikuweza kujua ni la kitu gani.
“Nikaondoka
pale pale kumfuata yule msichana aliyetoka mle ofisini ili nimuulize nini
kilitokea ndio hapo nilipomuona Waziri Mkuu na mke wake wamesimama mbele ya
mlango wakinitazama. Waziri Mkuu akaanza kunishutumu kuwa nimemfyonza damu
muuguzi wangu jambo ambalo si kweli”
“Sofia binti wa Waziri Mkuu
alikuwa amefuata nini ofisini kwako?” Thabit kembo, mmoja wa makachero
waliokuwa wakimhoji Dk Deo alimuuliza.
“Sijui”
“Je
wewe ulikutana na Waziri Mkuu alipofika hospitalini kwako?’
“Sikukutana
naye na wala sikuwa na taarifa kuwa waziri Mkuu anakuja hospitalini kwangu”
“Baada
ya Waziri Mkuu kukwambia kwamba amekuona umemfyonza damu muuguzi wako,
alichukua hatua gani?’
“Aliita
polisi wanikamate na hakunipa nafasi ya kujitetea”
ITAENDELEA kesho hapa hapa kumekucha.com