Wednesday, December 24, 2014

MVUA YA MAWE YASOMBA NYUMBA MIA MBILI, SINGIDA

Zaidi ya nyumba hamsini na moja zimebomolewa kwa Mvua kubwa huko Singida.


Zaidi ya nyumba hamsini na moja zimebomolewa kwa Mvua kubwa huko Singida.
News-shield-286711_640.jpg-pixabay (1)Zaidi ya nyumba hamsini na moja zinazo kadiriwa kuwa na wakazi zaidi ya miambili, katika Manispaa ya Singida, zimebomolewa na Mvua kubwa ya mawe iliyonyesha ikiambatana na upepo mkali.
Mvua hiyo iliyoanza kunyesha majira ya jioni imesababisha hasara kubwa kwa wakazi wa manispaa hiyo ambapo, mpaka sasa nyumba hamsini na moja zimeharibiwa ikiwemo Nyumba za watu binafsi na Madarasa ya Misikiti.
Mkuu wa Wilaya Qeen Mlozi amesema …”Serikali ya Mkoa kwa kweli mvua iliyonyesha jana takribani dakika kumi na tano paka ishirini ilikuwa mvua kubwa ya mawe na upepo mkal,  ambayo imesababisha  nyumba nyingi za mjini Singida zimeharibiwa na upepo, paka sasa wakati wataalam wanaendelea jumla ya nyumba hamsini na moja , zimeanguka, zimeharibiwa, zimeezuliwa na upepo
Ally Sanga Mkazi wa Singida amesema… “Imekuja mvua tuu mida ya jioni hii imedumu kama dakika 15 hivi alafu umekuja upepo mkali na mawe, ndio imesababisha madhara yote ambayo mnayaona imeangusha Nyumba, Miti, Nyaya za umeme zimekatika yani watu wana hali mbaya sana
Wakazi wa Manispaa hiyo wamesema Mvua iliyonyesha haijawahi kutokea pamoja na kunyesha kwa muda mfupi, lakini imeleta madhara makubwa sana na kulalamikia Manispaa ya Singida kwa kutokutengeneza vizuri miundombinu ya maji na kusababisha Nyumba nyingi kubomoka.
Hutopitwa na lolote na niko tayari kuutumia muda wangu kukuhabarisha kila jambo, kupitia kumekucha blog

No comments:

Post a Comment