Stori zilizopewa Headlines kwenye Magazeti ya leo Tanzania Dec 23, 2014 nimekuwekea hapa mtu wangu
MWANANCHI
Mgombea Uenyekiti wa kitongoji cha
Bujombe kwa tiketi ya CCM Ndengwe Mwakasoko ambaye alipita bila
kupingwa ameenguliwa baada ya kugundulika hajui kusoma wala kuandika.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri
hiyo Said Mderu alisema katika kitongoji cha Itete wagombea waliogongana
kura watafanya uchaguzi tena.
Alisena Mgombea huyo pekee wa CCM aliondolewa kwenye uchaguzi huo kwa sababu aikosa sifa hiyo.
Katibu wa CCM Wilaya ya Rungwe ambayo
inasimamia uchaguzi huo Marium Yusuph alipoulizwa kuhusu suala hilo
alikiri kuwepo kwa mgombea huyo aliyepitishwa kwa kishindo kwenye kura
za maoni za CCM huku akimlaumu Mtendaji wa kijiji kwa madai kwamba ndiye
aliyemwekea ‘kauzibe’.
MWANANCHI
Kashfa ya uchotwaji wa fedha za akaunti
ya Escrow imemwondoa kigogo wa pili baada ya jana Rais Kikwete kutangaza
kwamba atateua mtu mwingine kuchukua nafasi ya Waziri wa ardhi,nyumba
na maendeleo Makazi Prof. Anna Tibaijuka.
Tibaijuka anakua kiongozi wa pili
mwandamizi wa Serikali kuondoka madarakani kmwa kashfa hiyo baada ya
mwanasheria mkuu Jaji Fredrick Werema kujiuzulu hivi karibuni.
Aidha hatua hiyo inakuja baada ya hivi
katibuni Tibaijuka kuitisha mkutvano na waandishi wa habari na kusema
hawezi kujiuzulu kwa kuwa alichukua bilioni 1.6 kwa njia njema kutoka
kwa James Rugemalira wa VIP Engeneering na kwamba akifanya hivyo hadi
Rais atamshangaa.
Akiwahutubia wazee wa Jijini Dar es
salaam Kikwete alisema ‘Tumemuulizi Tibaijuka fedha hizo nyingi
amezipata vipi?akatujibu kwamba ni kwa ajili ya kuendesha shule,bodi ya
shule nayo ikatetea kwamba na shule ikatetea kwamba ni fedha za shule na
hiyo kwetu haina tatizo kusaidia shule,sisi hatukua na tatizo kwa nini
shule imepewa fedha tatizo lilikua kwanini fedha zimeingia kwenye
akaunti yake badala ya akaunti ya shule? alitujibu kuwa hayo ndiyo
masharti aliyopewa na Rugemarila…alisema Kikwete.
“Tukaona kwamba ,hapa kuna mapungufu,tukakubaliana na tukamwomba atuachie nafasi ili tumteue Waziri mwingine”Aliongeza.
MWANANCHI
Mamlaka ya usafiri wa majini na nchi
kavu SUMATRA imeruhusu mabasi ya usafiri jijini Dar es salaam maarufu
kama daladala kufanya safari za kwenda Mikoa ya Kaskazini kutokana na
mahitaji makubwa ya huduma hiyo katika kipindi hiki cha sikukuu za
krismas na mwaka mpya.
Mkurugenzi mkuu wa Sumatra Gilliard
Ngewe wamelazimika kuruhusu daladala hizo kukidhi mahitaji ya usafiri
kwenye mikoa ya Arusha na Kilimanjaro katika kipindi hiki.
Alisema wamefikia hatua hiyo baada ya
kuona wingi wa abiria wanaokwenda kwenye Mkoa hiyo ukilinganisha na
mabasi yaliyopo na pia Sumatra iko katika hatua za mwisho kuongeza
magari makubwa matano yanayofanya safari za Mikoa mingine ili
kukabiliana na hali hiyo.
“Kwa kweli ,hatukupanga kabisa kutumia
daladala hizo kuf anya safari za mbali,na ukiangalia kuna baadhi
daladala za Mbagala-Makumbusho tunazikagua hapa na kuzipa kibali kwa
ajili ya kuziruhusu kusafiri”alisema.
JAMBOLEO
Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Nyakabale
katika Wilayani Geita Josephat Msafiri amecharazwa viboko na akina mama
waliokwenda kupata huduma ya matibabu na kumkuta akiwa baa muda wa
kazi.
Wakinamama hao zaidi ya 20 waliofika
katika Zahanati hiyo wakiwa na watoto ambao ni wagonjwa na wengine
wakiwa wajawazito walimkuta daktari huyo akiwa baa huku Zahanati hiyo
ikiwa imefungwa.
Baada ya kumkuta akinywa pombe
walishikwa na hasira na kuanza kumchara viboko na alipolemewa na kipigo
hicho alikimbia na kujificha.
Akielezea sakata hilo mlinzi wa Zahanati
hiyo Kabunda Nyakiso alisema Mganga huyo tangu juzi alipokua zamu
alifika saa sita usiku akiwa amelewa na alipoulizwa alijibu kwa kejeli
huku aitoa maneno ya matusi.
NIPASHE
Askari mmoja wa jeshi la Polisi
amefariki dunia na wengine watano wamenusurika kufa baada ya boti
waliyokua wamepanda kwa ajili ya kufanya doria kupinduka katika Bahari
ya Hindi.
Ajali hiyo ilitokea juzi saa 7 usiku eneo la Jambiani,Kusini Unguja wakati askari hao wakiwa katika doria.
Kamanda wa Polisi Kusini Unguja Juma
Sadi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema boti hiyo ilikua na
askari sita wa kikosi cha kuzuia magendo Zanzibar KMKM.
Alisema wanne waliookolewa ni majeruhi na kwamba mmoja mpaka sasa hajapatikana.
“Hadi sasa bado askari mmoja
hajapatikana ambaye ni ASP Tenga na juhudi za kumtafuta
zinaendelea,,chanzo cha ajali inasemekana ni mashine za boti zilianza
kujaa maji kisha kupinduka na mawimbi yalichangia kwa kiasi kikubwa
kusababisha ajali hiyo” alisema.
NIPASHE
Maduka 100 yanayojishughulisha na uuzaji
wa dawa baridi katika jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela yamefungwa
kutokana na kukiuka sheria,kanuni na utaratibu wa kutoa dawa.
Mfamasia wa Jiji la MwanzaEdward
Magelewanya kutokana na zoezi hilo lililofanyika Disemba 8 hadi 20 mwaka
huu,wamiliki 10 kati ya hao walifikishwa mahakama ya hakimu mkazi
Nyamagana.
Alisema ukaguzi huo ulifanyika katika
maduka 171 kwa kushirikiana na idara za afya za jiji na Manispaa,ofisi
ya Mganga mkuu,waganga wakuub wa Wilaya na TFDA,TRA.
“Lengo ni kuangalia kama kama sheria,
kanuni,miongozo ,viwango na taratibu za kutoa dawa kwa sekta binafsi
zinzafatwa na kutekelezwa kwa wamiliki hao”alisema.
HABARILEO
Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro imetajwa
kuwa ipo hatarini kutoweka kutokana na mwingiliano wa watu kuwa mkubwa
huku idara nyingi zikiongozwa na watu wasiostahili kuongoza.
Naibu Waziri wa Maliasili ametoa rai kwa
Wizara ya Nishati na Madini kuhakikisha haitoi tena vibali
vinavyomaliza muda wake ndani ya Hifadhi ya Ziwa Manyara na hifadhi
nyingine ambazo baadhiya wachimbaji wanachimba madini ya aina
mbalimbali.
Akisoma maazimio ya maagizo hayo mbele
ya Waandishi wa habari Mweyekiti wa kamati ya Ardhi,maliasilina
Mazingira James Lembeli alisema hifadhi hiyo ipo hatarini kutoweka
kutokana na wingi wa watu pia suala la wakuu wa idara kuondolewa nalo
linachangia hifadhi hiyo kufa.
Alisema ingawa haiingilii maamuzi ya
bodi ya Ngorongoro lakini asilimia 80 ya wakuu wa Idara hawapo na idara
nyingi zinangozwa na watu wasiostahili kuongoza.
Alisema Ngorongoro ina matatizo makubwa hivyo ni lazima Serikali iwe makini kuhakikisha hifadhi hiyo haifi
HakunaStori itakayokupita mtu wangu,niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,kumekucha blog
No comments:
Post a Comment