WAHAMIAJI 900 WAFARIKI DUNIA BAADA YA MASHUA YAO KUZAMA BAHARINI!
Maiti
za wahamiaji waliozama baada ya mashua yao kupinduka nje ya pwani ya
Libya siku ya Jumamosi zikiwa katika meli ya Italia katika bandari ya
Malta.
Wahamiaji
900 wanadaiwa kufariki dunia wakiwemo watoto na wanawake, 28. Eneo
ambapo mashua hiyo ilizama lina kina kirefu na huenda abiria wengi
walikuwa wamekwama ndani ya mashua.
Umoja wa
Mataifa unasema kuwa njia kutoka kaskazini mwa Afrika kwenda Italia na
Malta imekuwa eneo hatari zaidi duniani na makundi ya uokoaji
yanastahili kuwa yanapiga doria eneo hilo.
Waziri mkuu wa Italia, Matteo Renzi, anasema kuwa mkutano wa dharura unahitajika kuandaliwa ili kuzungumzia suala hilo.
No comments:
Post a Comment