Umeipata hii ya Askari wa Uingereza kuugua kichaa? Kisa unajua ni nini? Iko hapa…
Kuna ishu ambayo ukiisikia kwa mtu
unaweza kuichukulia poa yani.. lakini ukikutana na story kamili lazima
ukae vizuri kuisikiliza ishu ikoje.
Hii nimekuta kwenye mtandao wa gazeti maarufu Uingereza, linaitwa The Independent..
wameandika ripoTi inayoonesha kwamba kuna kundi kubwa sana la Wanajeshi
wa Uingereza ambao wamegundulika kuumwa ugonjwa wa akili, sababu ya
ugonjwa huo ni dawa ambazo huwa zinatumiwa na Wanajeshi hao ili kuzuia
wasipate maambukizi ya Malaria !!
Dawa hizo zinaitwa Mefloquine au jina jingine Lariam..
tayari toka 2008 mpaka leo kuna wanajeshi karibu 1,000 ambao walipata
matatizo ya akili kutokana na kutumia dawa hizo wakiwa nje ya Uingereza
kupigana vita.
Athari nyingine baada ya kutumia dawa hizo ni pamoja na kupata stress, na wengine wanajiua kabisa!
Alastair Duncan ni Meja Jenerali Mstaafu wa Jeshi hilo ambae aliwahi kwenda kwenye vita Sierra Leone, yeye ni mmoja ya walioathirika kwa kupata tatizo la akili baada ya kutumia dawa hizo.
Sasa ishu iko hivi, tunajua wanajeshi
wakiwa kwenye kazi yao, hivi inakuaje unakutana nao wakati tayari
wameathiriwa na dawa hizo?
No comments:
Post a Comment