Mohamed Morsi
Mahakama
nchini Misri inatarajiwa kutoa hukumu kwenye kesi kadhaa zinazomkabili
rais wa zamani Mohammed Morsi ambaye aliondolewa madarakani na jeshi
mwaka 2013.
Anakabiliwa
na kesi pamoja na viangozi wengine wa kundi la Muslim Brotherhood kwa
kuwachochea wafuasi kumuua mwandishi wa habari na waandamanaji wa
upinzani wakati wa makabiliano nje ya Ikulu ya rais mwaka 2012.
Mawakili
wanamtetea Mosri wamasema kuwa huenda akakabiliwa na hukumu ya
kifo. Mamia ya wafuasi wa kundi la Muslim Brotherhood wamehukumiwa kifo
katika mikakati ya kukabiliana na kundi hilo lililopigwa marufuku na rais
wa sasa Abdul Fattah al-Sisi.
Kundi la Muslim Brotherhood limemlaumu rais kwa kutumia mahakama kama silaha
No comments:
Post a Comment