Tangakumekuchablog, Korogwe
CHAMA cha wananchi CUF Wilayani hapa,kimemtaka Mkuu wa Wlaya ya Korogwe Hafsa Mtasiwa kuingilia kati ili kuweza kuzipatia ufumbuzi
kero ambazo zimekuwa zikiwakabili wakazi wa kijiji cha Mkwakwani kata ya Mnyuzi
kutokana na halmashauri ya Wilaya ya Korogwe kushindwa kuzishughulikia.
Mkurugenzi wa haki za binadamu wa chama CUF Wilayani
Korogwe,Masoud Rashid Mohamed aliwaeleza waaandishi wa habari kuwa kwa
muda mrefu sasa wananchi wa kijiji cha Mkwakwani wamekuwa wakikabiliwa na
matatizo mengi ambapo halmashauri yao imewapuuza ikiwatelekeza.
Mohamed alisema,miongoni mwa matatizo hayo yalianza mwaka
2012 kwa Serikali ya kijiji cha Mkwakwani kuwataka wananchi wenye umri kati ya
miaka 18 – 50 kutozwa michango ya Tsh 2,400/=
kwa kila mwananchi wakielezwa kuwa watajengewa sekondari jambo ambalo halijaweza kufanyika.
Amelitaja tatizo jingine ni kwamba kila mwaka Kijiji hicho
cha Mkwakwani kimekuwa na utaratibu wa kupata fedha kiasi cha Tsh 550,000/=
kutoka msitu wa Ambangulu ambapo licha ya utaratibu huo kuendelea lakini cha
kushangaza wananchi hawajaweza kufahamu fedha zao kule zilikokopelekwa.
Pia Mohamed alisema kuwa wananchi wa kijiji cha Mkwakwani
wanakabiliwa na kero ya kutojua ni kwanini fedha zao kiasi cha Tsh 609,000/=
zinazotokana na ushuru kwa mwaka 2013/14 zimetumiwa kwenye vikao vya WDC huku
viongozi wa serikali ya kijiji wakihusishwa na uvunaji wa miti ya mivule.
Mkurugenzi huyo wa haki za binadamu wa CUF wilayani Korogwe
alisema waanchi wamekuwa wakifanya kila jitihada ili kupata haki zao lakini
wamegonga ukuta hatua ambayo imeusababisha uongozi wa CUF kumuandikia barua
mkuu wa wilaya ya Korogwe Hafsa Mtasiwa ili kuingilia kati suala hilo.
Alisema awali walimuandikia mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya wilaya ya Korogwe kumtaka kuwapatia maelezo juu ya yote ambayo
yamekuwa yakijitokeza kwenye kijiji cha Mkwakwani lakini tangu wakati huo mpaka
sa sa hakuna majibu yenye tija ambapo wananchi wameishia kupuuzwa.
Alisema mapungufu hayo yote yamekuwa yakigunduliwa na
wanachama wa CUF ambapo kwa kufuata taratibu za kisheria wamejaribu hata
kuwadhibiti wahalifu akitolea mfano wa tukio la kukamatwa kwa viongozi wa
serikali waluiohusishwa na kuyvuna miti ya mivule huku mpaka leo kukiwa hakuna
kesi.
Kutokana na hayo yote mkurugenzi huyo wa haki za binadamu wa
CUF amesema kwamba mpaka sasa wamekosa imani na uongozi wa halmashauri ya
wilaya ya Korogwe hali iliyowalazimu kuomba msaada wa mkuu wao wa wilaya ili
kuona namna ambavyo wananchi wanapata haki zao kwa misingi ya katiba.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Korogwe
Lukas Mweri alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu malalamiko hayo aliahidi
kuwasiliana na ngazi za chini kama ile ya kata na kijiji husika kujua chanzo
cha kero hizo na namna ambavyo zinaweza kumalizwa ili kuepusha lawama hizo kwa
umma.
Mwisho
|
Friday, April 3, 2015
MKUU WA WILAYA YA KOROGWE AOMBWA KUOKOA JAHAZI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment