Friday, April 3, 2015

KENYA BADO HALI NI TETE

Ripoti ya kinachoendelea Chuo kilichovamiwa Kenya.. Idadi ya vifo yaongezeka

Ke Attack
Hali bado sio shwari kwa wenzetu Kenya, jana taarifa kubwa iliyoripotiwa kwa siku nzima kutoka kwenye nchi hiyo ni ishu ya kuvamiwa kwa Chuo Kikuu cha Garissa, ambacho kiko karibu na mpaka wa nchi ya Somalia.
Wavamizi hao walivamia jana katika Chuo hicho na kuua walinzi wawili na baadae kuendelea kuwashambulia wanafunzi.
Idadi ya vifo iliyoripotiwa mpaka sasa ni watu 147, askari na Vikosi vya Jeshi la nchi hiyo wameendelea kuzunguka maeneo ya Chuo hicho.
Shambulio ni kubwa likifananishwa na tukio la uvamizi wa Mall Shop za Westgate, Nairobi Setember 2013 ambalo lilisababisha vifo vya watu 67 na wengine zaidi ya 170 kujeruhiwa.
Mpaka sasa wavamizi waliouawa ni wanne na mmoja wao amekamatwa.
Zaidi ya wanafunzi 500 walifanikiwa kutoka salama katika eneo hilo la Chuo.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment