Sio kila bunduki utakayotishiwa nayo ni ya ukweli, hichi kisa ni uthibitisho
Hakuna
mtu yoyote ambaye ana ujasiri wa kutoogopa silaha, ndio maana ukikutana
na story majambazi au wezi wameiba sehemu basi mara nyingi utakuta
silaha zimetumika.
Tumesikia uhalifu mwingi sana ukitokea
DAR na miji mingine mikubwa kwamba majambazi wanavamia sehemu wanaiba
kwa kutumia bunduki.. nimekutana nayo mitandaoni kwamba Cape Town
imetokea ya aina hii, taxi ilikuwa inatembea barabarani majambazi
wakatokea na gari nyingine wakaizuia taxi kwa mbele.
Wakashuka jamaa wawili toka kwenye gari
hiyo, wakawatishia bunduki watu waliokuwa kwenye taxi, wale watu
wakashuka alafu majambazi wakamfunga kamba dereva wa taxi, wakamuweka
kwenye buti wakaiba taxi na kuondoka nayo.
Polisi walifanikiwa kuwakamata baadae
majambazi hao, lakini kilichonishtua ni kwamba hivi unaweza kuamini
kwamba kile walichokionesha kama bunduki kumbe ilikuwa ni toy na sio
bunduki ya ukweli!!
Japo hawakumdhuru mtu yoyote wakati
wanaiba gari, silaha waliyotumia haikuwa bunduki ya ukweli.. Polisi
wanawashikilia kwa sababu walichokifanya tayari ni uhalifu.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment