Watoto wanafeli mitihani, hii ishu wazazi wameona ashirikishwe mganga wa kienyeji !!
Umewahi
kukutana na stori za ishu za wanafunzi kulalamika kwamba shuleni kuna
mauzauza?? Kenya imetokea.. watu wakaihusisha na imani za kishirikina
moja kwa moja.
Mbunge wa Kaloleni, Gunga Mwinga ilibidi
ashangae kidogo wakati ambapo alikaribishwa mgeni rasmi kwenye shughuli
ya graduation ya wanafunzi waliomaliza.. basi unaambiwa ombi la wazazi
lilikuwa moja tu, wanahitaji Mbunge afanye mpango wa kuwaletea mganga
ili kuondoa ushirikina ambao wanahisi upo kwenye shule hiyo.
Makamu Mkuu wa Shule hiyo, Richard Charo amesema wanafunzi hawafaulu kabisa mitihani ya kitaifa, wanaamini hiyo inasababishwa na nguvu ya uchawi… lakini Afisa Elimu Chigulu Mwarumba nae
wazo lake halikuwa mbali na hao waliotangulia, yeye akasema wanafunzi
wa shule hiyo wamekuwa wakisumbuliwa na nguvu za kishirikina na ofisi
yake imepokea malalamiko ya aina hiyo mara nyingi.
“Mambo
yanayoendelea shuleni hapa yanaogofya mno, wasichana wanaanguka hovyo
na kuzimia.. wanafunzi wanaanguka mitihani ya kitaifa, tulileta wahubiri
wawili lakini hakuna mabadiliko yoyote.. sasa itabidi tulete mtaalamu
wa kufukuza mapepo, ninaamini kuna kitu kilizikwa shuleni hapa ili
kuzuia wanafunzi wasifanye vyema,”>>> alisema Mwalimu Mkuu.
Malalamiko yao wanasema kwamba shule
hiyo ilianza kuwa na matokeo mabaya kwenye mitihani ya kitaifa miaka
mitano iliyopita, miaka ya nyuma hali ilikuwa poa kabisa.. wazazi hao
wamesema wanataka mganga ambaye atawasaidia kufukuza pepo wachafu.
Hutopitwa na habari yoyote inayonifikia na niko tayari kukutumia muda na wakati wowote kupitia hapa hapa www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment