Thursday, April 16, 2015

ANAEDAIWA KUTAKA KUMUUA MWANDANI WAKE, AJITOKEZA

Mwendelezo wa ile Scandle  ya msichana aliyetaka kuuawa na mpenzi wake baada ya kumkataa, leo kasikika mwanaume…

lonely13
Scandle  ya binti mmoja maeneo ya Msasani Dar, ambaye aliingia kwenye ugomvi na mpenzi wake.. akalalamika kwamba mpenzi wake alitaka kumnywesha kwa nguvu maji ya betri huku akitishia kumuua.
Chanzo cha ugomvi wanasema ni ishu ya msichana huyo kumkataa mwanaume baada ya kugundua kuwa ana mke.. siku ya tukio mwanaume huyo alimfuata nyumbani kwake, akamlazimisha kuingia ndani na kuaanza kumkaba huku akimnywesha maji ya betri.
Leo ni muendelezo ambapo mwanaume huyo amesikika… amesema aligundua msichana huyo alikuwa kwenye uhusiano na rafiki yake ambae ni mfanyabiashara mwenzake.. akamuibia fedha na kutoroka… mwanaume huyo anadai kwamba alimfuata ili amlipe pesa zake ndio abapo ugomvi wao ulianzia, jamaa akataka ajiue mbele ya mwanamke huyo baada ya kuanza ugomvi wa muda ,mrefu kati yao, msichana huyo alimnyang’anya maji hayo ndio maana yakamdhuru lakini hakuwa na lengo la kumnywesha.
Mwanaume huyo amesema msichana huyo amemgombanisha na mke wake  pamoja na marafiki zake, kwa sasa ameamua kurudi nyumbani kwao Ifakara na anaenda kujiua kutokana na kuchoshwa na mambo aliyofanyiwa na binti huyo kwa sababu alimpenda lakini ndio hivyo kambadilikia.

No comments:

Post a Comment